Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Umpende Jirani Yako?
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Septemba 15
    • Kisha, huyo aliyemsaili Yesu akauliza hivi: “Na jirani yangu ni nani?” Badala ya kujibu moja kwa moja, Yesu alitoa hadithi yenye kielezi juu ya mwanamume wa Kiyahudi aliyekuwa amenyang’anywa mali, akapigwa, na kuachwa akiwa karibu kufa. Ndipo Wayahudi wawili wakaja—kwanza kuhani kisha Mlawi. Wote wawili walitazama hali ya yule Myahudi mwenzao lakini hawakufanya lolote kumsaidia. Halafu Msamaria akaja. Akisukumwa na huruma, alifunga majeraha ya Myahudi huyo aliyeumia, akampeleka kwenye nyumba ya wageni, na kufanya maandalizi ili atunzwe zaidi.

      Yesu alimuuliza hivi, huyo aliyemsaili: “Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?” Kwa wazi, alikuwa yule Msamaria mwenye rehema. Hivyo Yesu alionyesha kwamba kumpenda jirani kikweli hupita vizuizi vya kikabila.—Luka 10:29-37.

  • Kumpenda Jirani Kwawezekana
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Septemba 15
    • Kielelezo Chema cha Yesu

      Wayahudi wa karne ya kwanza walikuwa na hisia za chuki dhidi ya Wasamaria, watu walioishi katika eneo fulani kati ya Yudea na Galilaya. Katika pindi moja wapinzani wa Kiyahudi walimuuliza Yesu hivi kwa dharau: “Je! sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo? (Yohana 8:48) Mwelekeo wa kuwachukia Wasamaria ulikuwa wenye nguvu sana hivi kwamba Wayahudi fulani hata waliwalaani Wasamaria hadharani katika masinagogi na kusali kila siku kwamba Wasamaria wasipewe uhai wa milele.

      Bila shaka kujua juu ya chuki hiyo yenye kina kirefu kulimchochea Yesu kutoa kile kielezi juu ya Msamaria aliyejithibitisha kuwa jirani wa kweli kwa kumtunza yule mwanamume wa Kiyahudi aliyepigwa na wanyang’anyi. Yesu angalijibuje wakati yule mwanamume wa Kiyahudi aliyezoeleana na Sheria ya Kimusa alipomuuliza: “Na jirani yangu ni nani?” (Luka 10:29) Yesu angaliweza kujibu moja kwa moja kwa kusema: ‘Jirani yako anatia ndani Myahudi mwenzako na pia watu wengine, hata Msamaria.’ Hata hivyo, Wayahudi wangaliona ni vigumu kukubali jambo hilo. Kwa hiyo alisimulia kile kielezi cha Myahudi aliyepokea rehema ya Msamaria. Hivyo Yesu aliwasaidia wasikilizaji wa Kiyahudi wafikie mkataa kwamba kupenda jirani kikweli kungeonyeshwa kwa wasio Wayahudi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki