Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Katika Hatari za Baharini”
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • Kwa kuwa walikosa vifaa—hata dira—mabaharia wa karne ya kwanza waliendesha meli hasa kwa kutumia macho. Kwa hiyo, usafiri ulikuwa salama zaidi wakati hali ya kuona ilipokuwa nzuri kabisa—kwa ujumla kuanzia mwisho-mwisho wa Mei hadi katikati ya Septemba. Wakati wa miezi miwili ya kabla na baada ya wakati huo, huenda wafanya-biashara wangejasiria kusafiri. Lakini wakati wa majira ya baridi, mara nyingi ukungu na mawingu vilisitiri alama za ardhini na jua wakati wa mchana, na nyota wakati wa usiku. Usafiri wa baharini ulionwa kuwa umefungwa (Kilatini, mare clausum) kuanzia Novemba 11 hadi Machi 10, isipokuwa katika hali za lazima kabisa au za dharura. Wale waliosafiri wakiwa wamechelewa wakati wa majira hayo walikabili hatari ya kukaa katika bandari ya ugenini wakati wa majira ya baridi.—Matendo 27:12; 28:11.

  • “Katika Hatari za Baharini”
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • Kwa wazi, Paulo alijua hatari za kusafiri baharini wakati wa majira yasiyofaa. Hata alitoa shauri dhidi ya kusafiri mwisho-mwisho wa Septemba au mapema Oktoba, akisema hivi: “Wanaume, nahisi kwamba uendeshaji utakuwa na dhara na hasara kubwa si ya shehena na mashua tu bali pia ya nafsi zetu.” (Matendo 27:9, 10) Hata hivyo, ofisa-jeshi aliyeshika usukani akayapuuza maneno hayo, na jambo hilo likatokeza kuvunjikiwa meli huko Malta.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki