Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Januari 15
    • Farasi wa Rangi Nyekundu

      Mmoja wa farasi walioonwa na Yohana alikuwa “mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.”​—Ufunuo 6:4.

      “Upanga mkubwa” wa mpanda farasi huyu unafananisha vita. Kwa hiyo, tangu 1914 watu milioni 69 hivi walikufa katika vita vya ulimwengu viwili. Hayo yalikuwa mauaji makubwa kama nini! Kweli kweli, umati mkubwa wa wajane, na yatima unashuhudia kwamba mpandaji wa farasi mwekundu, anayefananisha vita vya kimataifa, amekuwa na matokeo ya moja kwa moja maishani mwao.

      Zaidi ya hayo, vita vyenye kuendelea na matisho ya vita vinalemeza sana kizazi cha vijana. Katika nchi ambazo kuna mapambano yenye moto, matineja ndio wanaopigana kwa sehemu kubwa. Matokeo ya vita juu ya vijana hawa yanaelezwa kwa maneno machache katika ulizo hili lililotolewa na mwenyekiti wa shirika moja la kutetea haki za kibinadamu: “Wawezeje kukua wakiwa timamu na watu wazima waliosawazika?”

      Vijana katika nchi mbalimbali wanaopatwa moja kwa moja na matokeo ya vita wamejifunza kuhesabu wakati kuwa saa na siku badala ya miezi na miaka. Wanauliza: “Baadaye, ni nani anayejali juu ya baadaye? Unaweza kutoa uhakikisho kwamba kombora halitapiga chumba changu usiku wa leo niendapo kulala?”

      Namna gani watoto wanaoishi katika nchi zenye amani? Je, wanapatwa na matokeo ya vita vya yule mpanda farasi? Ndiyo, tisho lenye huzuni la vita ya nyukilia limekuwa na matokeo makubwa ya kiakili juu yao. Kuhusu kukata tumaini kulikoonyeshwa na wanafunzi wake, mwalimu mmoja wa kike alitamka hivi: “Niliposikia maelezo hayo tena na tena nilikumbwa na hisia ya kutokuamini. Watoto hawa wachanga walihisi kadiri ya kukata tumaini nisiyojiruhusu mwenyewe kuhisi.” Dakt. Richard Logan wa Quebec, Kanada, aliongeza hivi: “Kujiona hoi na bila uwezo ndio ufafanuzi wa utaalamu wa matatizo ya akili kuhusu kushuka moyo. Hilo ndilo tunaloona katika vijana wengi.”

      Lakini namna gani ikiwa huishi katika nchi yenye vita au huhisi tatizo hilo linageuza maono yako ya ndani? Bado mpandaji wa farasi mwekundu anakuwa na matokeo maishani mwako. Kila dakika dola milioni 1.3 zinatumiwa kwa makusudi ya moja kwa moja ya kijeshi​—dola kama elfu milioni 660 kwa mwaka ulimwenguni pote. Ni nani anayelipia hizo zote? Ni wewe. Po pote unapoishi, matokeo ya mpandaji wa farasi mwekundu yanakupata.

  • Wapanda Farasi wa Kitabu cha Ufunuo—Jinsi Unavyopatwa na Matokeo ya Upandaji Wao
    Mnara wa Mlinzi—1986 | Januari 15
    • FARASI MWEKUNDU: Mpandaji farasi huyo anafananisha vita. Amani inaondolewa duniani, na kutokea vita ya ulimwengu kunatiwa alama.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki