-
Matetemeko ya Dunia Katika Siku ya BwanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
26. Binadamu wanaopinga enzi kuu ya Mungu watatendaje katika hofu yao, na ni maneno gani ya hofu kuu watakayotamka?
26 Maneno ya Yohana yanaendelea: “Na wafalme wa dunia na wenye vyeo vya juu na makamanda wa kivita na matajiri na makamambe na kila mtumwa na kila mtu huru wakajificha wenyewe katika mapango na katika yale matungamo-miamba ya milima. Na wao walifuliza kusema kwa milima na kwa matungamo-miamba: ‘Angukeni juu ya sisi na kuficha sisi kutoka uso wa yule Mmoja aliyeketi juu ya kiti cha ufalme na kutoka hasira-kisasi ya Mwana-Kondoo, kwa sababu siku kubwa ya hasira-kisasi yao imekuja, na ni nani anaweza kusimama?’”—Ufunuo 6:15-17, NW.
-
-
Matetemeko ya Dunia Katika Siku ya BwanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
30. (a) Ni nini kinachodokezwa na swali hili: “Ni nani anaweza kusimama?” (b) Je! wowote wataweza kusimama wakati wa hukumu ya Yehova?
30 Ndiyo, wale ambao wamekataa kutambua mamlaka ya yule Mpandaji-farasi mweupe mwenye ushindi watalazimika kukubali kosa lao. Wanadamu ambao kwa kupenda wamekuwa mbegu ya yule nyoka wataelekeana na uharibifu wakati ulimwengu wa Shetani unapopitilia mbali. (Mwanzo 3:15; 1 Yohana 2:17) Hali ya ulimwengu kwenye wakati huo itakuwa ya aina ya kwamba, ni kana kwamba wengi watakuwa wakiuliza: “Ni nani anaweza kusimama?” Yaonekana kama watadhani hakuna yeyote kwa vyovyote ambaye anaweza kusimama akiwa anakubalika mbele za Mungu katika siku hiyo ya hukumu yake. Lakini watakuwa wenye kukosea, kama vile kitabu cha Ufunuo kinavyoendelea kuonyesha.
-