Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ole wa Kwanza—Nzige
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 13. Nzige wana mwonekano gani?

      13 Lo! nzige hao wana mwonekano wa kutazamisha kama nini! Yohana anaeleza habari yao: “Na mifanano ya nzige ilishabihi farasi walio tayari kwa ajili ya pigano; na juu ya vichwa vyao palikuwa na kilichoonekana kuwa mataji kama dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu, lakini walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama yale ya masimba; na walikuwa na mabamba-kifua kama mabamba-kifua ya chuma. Na mvumo wa mabawa yao ulikuwa kama mvumo wa magari ya farasi wengi wenye kukimbia kuingia ndani ya pigano.”—Ufunuo 9:7-9, NW.

  • Ole wa Kwanza—Nzige
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 15. Ni jambo gani linalomaanishwa na (a) mabamba-kifua ya chuma ya hao nzige? (b) nyuso kama za wanadamu? (c) nywele kama za wanawake? (d) meno kama yale ya masimba? (e) kufanya kelele nyingi?

      15 Katika njozi, hao nzige wana mabamba-kifua ya chuma, kufananisha uadilifu usiovunjika. (Waefeso 6:14-18) Pia wao wana nyuso kama za wanadamu, sura hii ikielekeza kwenye sifa ya upendo kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, ambaye ni upendo. (Mwanzo 1:26; 1 Yohana 4:16) Nywele zao ni ndefu kama za mwanamke, ambazo hutoa vizuri picha ya utii wao kwa Mfalme wao, “malaika wa abiso.” Na meno yao hushabihi meno ya simba. Simba hutumia meno yake kurarua nyama. Tangu 1919 na kuendelea, jamii ya Yohana imekuwa ikiweza kutwaa chakula kigumu cha kiroho, hasa zile kweli juu ya Ufalme wa Mungu unaotawalwa na “simba ambaye ni wa kabila la Yuda,” Yesu Kristo. Kama vile simba hufananisha ushujaa, ndivyo ushujaa mwingi umekuwa ukihitajiwa ili kuyeyusha tumboni huu ujumbe wenye kupiga sana, kuutia katika vichapo, na kuugawanya kuzunguka tufe lote. Nzige hao wa kitamathali wamefanyiza kelele nyingi, kama “mvumo wa magari ya farasi wengi wenye kukimbia kuingia ndani ya pigano.” Wakifuata kielelezo cha Wakristo wa karne ya kwanza, wao hawakusudii kukaa kimya.—1 Wakorintho 11:7-15; Ufunuo 5:5, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki