-
Kazi za Yehova—Kubwa na za AjabuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
14. Ni nani ambao Yohana huona wakiibuka kutoka patakatifu, na wanapewa nini?
14 Inafaa tusikie wimbo wa hawa washindi wapakwa-mafuta. Kwa nini? Kwa sababu wametangaza peupe duniani hukumu zilizokuwa katika mabakuli yaliyokuwa yamejaa kasirani ya Mungu. Lakini kumiminwa kwa mabakuli haya kunahusu zaidi ya binadamu wa vivi hivi tu, kama Yohana aendeleavyo kuonyesha: “Na baada ya vitu hivi mimi nikaona, na patakatifu pa hema ya ushahidi palifunguliwa katika mbingu, na malaika saba wakiwa na tauni saba waliibuka kutoka patakatifu, wakiwa wamevaa kitani safi, nyangavu na wamefunga kifuani mishipi ya dhahabu. Na mmoja wa viumbe hai wanne akawapa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyokuwa yamejaa kasirani ya Mungu, ambaye huishi milele na milele.”—Ufunuo 15:5-7, NW.
-
-
Kazi za Yehova—Kubwa na za AjabuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
16. (a) Ni nini kinachoonyesha kwamba hao malaika saba wanastahili sana kufanya kazi yao? (b) Ni nini kinachoonyesha kwamba wengine wanahusika katika hii kazi kubwa ya kumimina mabakuli ya ufananisho?
16 Malaika hawa wanastahili sana kufanya kazi hii. Wao wanavaa kitani safi, nyangavu, kuonyesha kwamba wao ni safi kiroho na ni watakatifu, waadilifu katika mwono wa Yehova. Pia, huvaa mishipi ya dhahabu. Kwa kawaida mishipi inatumiwa wakati mtu anapojifunga mwenyewe kwa ajili ya kazi inayopasa kutimizwa. (Walawi 8:7, 13; 1 Samweli 2:18; Luka 12:37; Yohana 13:4, 5) Kwa hiyo malaika wamejifunga mishipi kwa ajili ya kutimiza mgawo. Zaidi ya hayo, mishipi yao ni ya dhahabu. Katika tabenakulo ya kale, dhahabu ilitumiwa kuwakilisha vitu vya kimungu, vya kimbingu. (Waebrania 9:4, 11, 12) Hiyo inamaanisha kwamba malaika hawa wana utume wa utumishi wa kimungu, wenye thamani sana kuufanya. Wengine wanahusika vilevile katika kazi hii kubwa. Mmoja wa viumbe hai wanne anawapa mabakuli yenyewe. Pasipo shaka, huyu alikuwa kiumbe hai wa kwanza, ambaye alishabihi simba, kufananisha ujasiri na ushujaa usiotishika unaohitajiwa ili kupiga mbiu ya hukumu za Yehova.—Ufunuo 4:7, NW.
-