Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sikukuu ya Kuzaliwa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • “Wagiriki waliamini kwamba kila mtu alikuwa na roho au daemon mwenye kumlinda aliyekuwapo wakati wa kuzaliwa kwake na kumlinda maishani. Roho huyo alikuwa na uhusiano wa kifumbo pamoja na mungu ambaye mtu huyo alizaliwa katika sikukuu yake ya kuzaliwa. Waroma pia waliunga mkono wazo hilo. . . . Wazo hilo liliendelezwa katika imani ya binadamu na linaonekana katika malaika mlinzi, mama wa ubatizo na mtakatifu mlezi. . . . Desturi ya kuwasha mishumaa juu ya keki ilianzishwa na Wagiriki. . . . Keki za asali za mviringo kama mwezi na zenye kuwashwa kwa mishumaa midogo ziliwekwa juu ya madhabahu za hekalu la [Artemi]. . . . Mishumaa ya sikukuu za kuzaliwa, katika hekaya za watu, ina uwezo wa pekee wa kuwapa watu yale wanayotamani. . . . Mishumaa midogo iliyowashwa na mioto ya dhabihu imekuwa na maana ya pekee ya kifumbo tangu mwanadamu alipoisimamishia miungu yake madhabahu mara ya kwanza. Kwa hiyo mishumaa ya sikukuu ya kuzaliwa ni heshima na sifa kwa mtoto wa sikukuu hiyo ya kuzaliwa na huleta bahati njema. . . . Salamu za sikukuu ya kuzaliwa na heri njema ni sehemu muhimu ya sikukuu hiyo. . . . Mwanzoni wazo hilo lilianzia katika uchawi. . . . Salamu za sikukuu ya kuzaliwa zinaweza kuleta mema au mabaya kwa sababu mtu huwa karibu zaidi na ulimwengu wa roho katika siku hiyo.”—The Lore of Birthdays (New York, 1952), Ralph na Adelin Linton, uku. 8, 18-20.

      Si vibaya familia na marafiki kukusanyika ili kula, kunywa, na kufurahi

      Mhu. 3:12, 13: “Hakuna jambo lingine bora kwao kuliko mtu kufurahi na kufanya mema maishani mwake; na pia kwamba kila mtu ale, naam, anywe na kuona mema kwa ajili ya kazi yake yote iliyo ngumu. Hiyo ndiyo zawadi ya Mungu.”

      Ona pia 1 Wakorintho 10:31.

  • Siku za Mwisho
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Siku za Mwisho

      Maana: Biblia hutumia maneno haya “siku za mwisho” kurejezea kipindi cha kumalizia kinachoelekeza kwenye kutekelezwa kwa hukumu iliyowekwa na Mungu. Huo ndio utakaokuwa mwisho wa mfumo wa mambo. Siku za mwisho za mfumo wa Kiyahudi pamoja na ibada yake iliyotegemea hekalu la Yerusalemu zilifika kati ya mwaka wa 33 mpaka 70 W.K. Mambo yaliyotukia wakati huo yanafanana na mambo ambayo yangetimia kwa kiwango kikubwa zaidi ulimwenguni pote wakati ambapo mataifa yote yatakabili kutekelezwa kwa hukumu ya Mungu. Siku za mwisho za mfumo mbovu wa mambo uliopo, wa ulimwenguni pote, zilianza mwaka wa 1914.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki