-
2 Samweli 23:11, 12Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
11 Aliyemfuata ni Shamma mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walikusanyika kule Lehi, mahali ambapo palikuwa na shamba lililojaa dengu; na watu wakakimbia kwa sababu ya Wafilisti. 12 Lakini alisimama katikati ya shamba hilo na kuwazuia Wafilisti wasiingie humo, naye aliendelea kuwaua Wafilisti, hivi kwamba Yehova akawapa ushindi* mkubwa.+
-