Wagalatia
4 Basi nasema kwamba maadamu mrithi ni kitoto hatofautiani hata kidogo na mtumwa, ingawa yeye ni bwana wa vitu vyote, 2 bali yeye yuko chini ya watu wenye kusimamia na chini ya wasimamizi-nyumba hadi siku ambayo baba yake aliweka kimbele. 3 Hivyohivyo sisi pia, tulipokuwa vitoto, tuliendelea kufanywa watumwa na mambo ya msingi yaliyo ya ulimwengu. 4 Lakini kikomo kamili cha wakati kilipowasili, Mungu alimtuma Mwana wake, aliyekuja kuwa kutokana na mwanamke na aliyekuja kuwa chini ya sheria, 5 ili apate kuachilia kwa kununua wale walio chini ya sheria, ili sisi, nasi, tupate kupokea tendo la kufanywa kuwa wana.
6 Sasa kwa sababu nyinyi ni wana, Mungu ametuma roho ya Mwana wake ndani ya mioyo yetu nayo hupaaza kilio: “Abba, Baba!” 7 Basi, kwa hiyo wewe si mtumwa tena bali mwana; na ikiwa ni mwana, pia ni mrithi kupitia Mungu.
8 Hata hivyo, mlipokuwa hammjui Mungu, wakati huo ilikuwa kwamba mlitumikia kama watumwa wale ambao kwa asili si miungu. 9 Lakini sasa kwa kuwa mmekuja kumjua Mungu, au afadhali zaidi kusema kwa kuwa sasa mmekuja kujulikana na Mungu, ni jinsi gani kwamba mnarudia tena mambo ya msingi yaliyo dhaifu na yasiyo na maana na kutaka kuyatumikia mkiwa watumwa kwa mara nyingine tena? 10 Kwa uangalifu mwingi mno mnazishika siku na miezi na majira na miaka. 11 Mimi nawahofia, kwamba kwa njia fulani nimemenyeka bila kusudi lolote kwa habari yenu.
12 Akina ndugu, nawaomba nyinyi, Iweni kama nilivyo, kwa sababu mimi nilikuwa pia na kawaida ya kuwa kama mlivyo. Hamkunitenda kosa lolote. 13 Lakini mwajua kwamba ilikuwa kupitia ugonjwa wa mwili wangu kwamba niliwatangazia nyinyi habari njema mara ya kwanza. 14 Na lililokuwa jaribu kwenu katika mwili wangu, hamkulitendea kwa dharau au kulitemea mate kwa kuchukizwa sana; bali mlinipokea mimi kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu. 15 Basi, iko wapi furaha mliyokuwa nayo? Kwa maana nawatolea nyinyi ushahidi kwamba, kama ingaliwezekana, mngaling’oa kabisa macho yenu na kunipa hayo. 16 Hivyo basi, je, nimekuwa adui yenu kwa sababu nawaambia nyinyi kweli? 17 Wao wawatafuta nyinyi kwa bidii, si katika njia bora, bali wataka kuwazuia nyinyi kutoka kwangu, ili mpate kuwatafuta wao kwa bidii. 18 Hata hivyo, ni bora kwenu kuwa wenye kutafutwa kwa bidii kwa sababu bora nyakati zote, na si wakati tu mimi niwapo pamoja nanyi, 19 watoto wangu wadogo, ambao mimi ni pamoja nao tena katika maumivu ya kuzaa mtoto mpaka Kristo afanyike katika nyinyi. 20 Lakini ningeweza kutaka kuwapo pamoja nanyi sasa hivi na kusema katika njia tofauti, kwa sababu nafadhaishwa juu yenu.
21 Mniambie, nyinyi mtakao kuwa chini ya sheria, Je, hamsikii Sheria? 22 Kwa kielelezo, imeandikwa kwamba Abrahamu alijipatia wana wawili, mmoja kwa njia ya msichana-mtumishi na mmoja kwa njia ya mwanamke huru; 23 lakini yule kwa msichana-mtumishi kwa kweli alizaliwa katika namna ya mwili, yule mwingine kwa mwanamke huru kupitia ahadi. 24 Mambo haya yasimama kama drama ya ufananisho; kwa maana wanawake hawa wamaanisha maagano mawili, lile moja kutoka Mlima Sinai, ambalo huzaa watoto kwa ajili ya utumwa, na ambalo ni Hagari. 25 Basi Hagari huyu amaanisha Sinai, mlima ulio Arabuni, naye alingana na Yerusalemu la leo, kwa maana liko katika utumwa pamoja na watoto walo. 26 Lakini Yerusalemu la juu ni huru, nalo ni mama yetu.
27 Kwa maana imeandikwa: “Uwe na mteremo, wewe mwanamke tasa usiyezaa; bubujika hisia na lia kwa sauti kubwa, wewe mwanamke usiyekuwa na maumivu ya kuzaa mtoto; kwa maana watoto wa mwanamke aliye mkiwa ni wengi zaidi sana kuliko wale wa yeye aliye na mume.” 28 Basi, akina ndugu, sisi ni watoto wa ahadi vilevile kama Isaka alivyokuwa. 29 Lakini kama vile yule aliyezaliwa katika namna ya mwili alipoanza kumnyanyasa yeye aliyezaliwa katika namna ya roho, ndivyo ilivyo pia na sasa. 30 Hata hivyo, Andiko lasema nini? “Fukuza msichana-mtumishi na mwana wake, kwa maana hakika mwana wa msichana-mtumishi hatakuwa mrithi kwa vyovyote pamoja na mwana wa mwanamke huru.” 31 Kwa sababu hii, akina ndugu, sisi ni watoto, si wa msichana-mtumishi, bali wa mwanamke huru.