Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Mambo ya Nyakati 19:1-5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 19 Baadaye Nahashi mfalme wa Waamoni akafa, na mwanawe akawa mfalme baada yake.+ 2 Ndipo Daudi akasema: “Nitamtendea kwa upendo mshikamanifu+ Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea kwa upendo mshikamanifu.” Basi Daudi akawatuma wajumbe ili wamfariji baada ya kufiwa na baba yake. Lakini watumishi wa Daudi walipofika katika nchi ya Waamoni+ kumfariji Hanuni, 3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni: “Je, unafikiri kwamba Daudi anawatuma wafariji kwako ili kumheshimu baba yako? Je, watumishi wake hawajaja kwako ili kufanya uchunguzi kamili na kukupindua wewe na kuipeleleza nchi?” 4 Kwa hiyo Hanuni akawachukua watumishi wa Daudi, akawanyoa,+ akakata nguo zao katikati kwenye matako na kuwafukuza. 5 Daudi alipoambiwa kuhusu wanaume hao, mara moja akawatuma wanaume wengine waende kukutana nao, kwa sababu wanaume hao walikuwa wameaibishwa sana; mfalme akawaambia: “Kaeni Yeriko+ mpaka ndevu zenu zitakapoota, kisha mrudi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki