-
2 Samweli 10:1-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Baadaye mfalme wa Waamoni+ akafa, na Hanuni mwanawe akawa mfalme baada yake.+ 2 Ndipo Daudi akasema: “Nitamtendea kwa upendo mshikamanifu Hanuni mwana wa Nahashi kama baba yake alivyonitendea kwa upendo mshikamanifu.” Basi Daudi akawatuma watumishi wake ili wamfariji baada ya kufiwa na baba yake. Lakini watumishi wa Daudi walipofika katika nchi ya Waamoni, 3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao: “Je, unafikiri kwamba Daudi anawatuma wafariji kwako ili kumheshimu baba yako? Je, Daudi hajawatuma watumishi wake ili kulichunguza jiji lote na kulipeleleza na kuliteka?” 4 Kwa hiyo Hanuni akawachukua watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao,+ akakata nguo zao katikati kwenye matako na kuwafukuza. 5 Daudi alipoambiwa habari hiyo, mara moja akawatuma wanaume fulani waende kukutana nao, kwa sababu watumishi hao walikuwa wameaibishwa sana; mfalme akawaambia: “Kaeni Yeriko+ mpaka ndevu zenu zitakapoota, kisha mrudi.”
-