-
Ezekieli 5:12, 13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Theluthi yenu moja watakufa kwa ugonjwa hatari au kuangamia kwa njaa kali miongoni mwenu. Na theluthi nyingine watauawa kwa upanga kuwazunguka pande zote.+ Nami nitaitawanya theluthi ya mwisho kila upande,* nami nitauchomoa upanga ili kuwakimbiza.+ 13 Ndipo hasira yangu itakapokoma, na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitaridhika.+ Nitakapomaliza kuwamwagia ghadhabu yangu, watalazimika kujua kwamba mimi, Yehova, ninasisitiza watu waniabudu mimi peke yangu.+
-