-
Mathayo 21:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Walipokaribia Yerusalemu na kufika Bethfage kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wanafunzi wawili,+ 2 akawaambia: “Nendeni katika kijiji mtakachokiona, na mara moja mtamwona punda amefungwa, na mwanapunda akiwa pamoja naye. Wafungueni na kuniletea. 3 Mtu yeyote akiwauliza, semeni, ‘Bwana anawahitaji.’ Na mara moja atawaruhusu mwachukue.”
-
-
Luka 19:29-34Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
29 Alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye Mlima wa Mizeituni,+ akawatuma wawili kati ya wanafunzi,+ 30 akisema: Nendeni katika kijiji mtakachokiona, na mtakapoingia mtamwona mwanapunda akiwa amefungwa, ambaye hakuna mtu amewahi kuketi juu yake. Mfungueni na kumleta. 31 Lakini mtu akiwauliza, ‘Kwa nini mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.’” 32 Basi wale waliotumwa wakaenda na kupata sawasawa na vile Yesu alivyowaambia.+ 33 Lakini walipokuwa wakimfungua mwanapunda huyo, wenyewe wakawauliza: “Mbona mnamfungua huyo mwanapunda?” 34 Wakajibu: “Bwana anamhitaji.”
-