Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 11/8 uku. 2
  • Ukurasa wa Pili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukurasa wa Pili
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Bunduki Tele
Amkeni!—1990
g90 11/8 uku. 2

Ukurasa wa Pili

Bunduki Tele

Bunduki zikizidi, mifyatuo itazidi, mauaji yatazidi. Katika United States mfyatua-bunduki anyunyizia umati wa watoto wa shule risasi mia moja kutokana na bunduki ya ushambulizi ya kumimina risasi haraka: 5 wafa, 29 wajeruhiwa. Katika Uingereza mwanamume kichaa aua kinyama watu 16 kwa bunduki ya ushambulizi ya aina ya AK-47. Katika Kanada mwanamume mmoja achukiaye wanawake aenda Chuo Kikuu cha Montreal na kuua 14 wa hao. Katika San Salvador walinzi wazunguka-zunguka katika vijia vya sokokuu wakiwa na bunduki za aina ya shotigani, na wanunuzi watakwa waache silaha zao mlangoni.

Wanawake zaidi sasa wananunua bunduki. Wao wamiminika kwa wingi kwenye sehemu za kulenga shabaha za bastola na bunduki, wakifyatua-fyatua risasi katika shabaha zinazofanana na wanaume halisi, wakitoboa matundu katikati ya macho yao kwa risasi. Bastola zilizoundwa kwa njia maalumu kwa ajili ya wanawake zinanunuliwa sana.

Na usiwasahau watoto. Kisa kimoja kati ya vingi: Mvulana wa miaka kumi “alitia risasi katika bunduki yenye nguvu nyingi ya mawindo ya baba yake na kumfyatulia hadi kifo msichana aliyekuwa amejigamba kuwa bora kuliko yeye katika michezo ya vidio.”

Shindano la kutumia silaha nyumbani laendelea. Litaishia wapi? Litaisha lini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki