Ukurasa wa Pili
Lile Teketezo la Umati—Ni Nani Waliosema kwa Ujasiri?
Sherehe ya Kuadhimisha Mwaka wa 50 wa Kuziweka Huru Kambi 3-15
Miaka 50 iliyopita wale walioweka huru kambi za mateso za Nazi walipatwa na ogofyo kwa kile walichoona. Sauti moja ilikuwa imekuwa ikitangaza ukatili wa Nazi kwa miaka mingi. Lakini ni nani walioshindwa kusema kwa ujasiri? Kwa nini walikuwa kimya? Makala hizi zatia ndani habari iliyotolewa kwenye semina iliyofanywa katika Jumba la Kuhifadhia Vitu vya Kale vya Teketezo la Umati, Washington, D.C., Marekani.
Nidhamu Imekuwa Wokovu Wangu 19
Jifunze jinsi maisha ya mapema ya nidhamu ya mwanamke fulani yalimsaidia kushinda matatizo magumu.
Msiba wa Ghafula wa Japani—Jinsi Watu Walivyoukabili 22
Zaidi ya watu 5,000 walikufa katika tetemeko la dunia la Kobe lenye maafa. Mashahidi wa Yehova walikabilije hali huko? Je, tunapasa kushangazwa na matetemeko ya dunia yenye kutokeza uharibifu?