Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w76 5/1 kur. 195-197
  • Maisha Yasiyo na Udhalimu—Je! Ni Ndoto Tu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maisha Yasiyo na Udhalimu—Je! Ni Ndoto Tu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • JINSI “NDOTO” ITAKAVYOKUWA JAMBO HALISI
  • Je, Kilio cha Haki Kitasikika?
    Habari Zaidi
  • Je! Kweli Kuna Wakati Ambapo Mungu Ataondoa Ukosefu wa Haki?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Yehova Ni Mpenda-haki
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • “Njia Zake Zote Ni Haki”
    Mkaribie Yehova
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
w76 5/1 kur. 195-197

Maisha Yasiyo na Udhalimu​—⁠Je! Ni Ndoto Tu?

JE! DUNIA isingekuwa mahali pa kupendeza zaidi kuishi kama watu wote, na hasa wenye mamlaka, wangekuwa wasiopendelea na wenye haki kabisa? Katika siku zetu kuna tumaini gani la kuona ulimwengu usio na udhalimu? Ungeweza kupatikanaje?

Kutokana na tunayoona kutuzunguka, huenda kukaelekea kutokuwa na matumaini mengi ya kuupata ulimwengu huo. Fikiria mifano michache ya mambo yanayokasirisha wengi mno na kuwafanya wajione bila tumaini.

Kwanza, watu wanaona matajiri na maafisa wakuu wa serikali wakivunja sheria na mara nyingi wakiponyoka. Pengine wao hulipa faini ndogo tu.

Kwa mfano, wakati kampuni moja ya New York yenye kushughulika na kufanya mikataba ya uuzaji na ununuzi ilipoiba bidhaa za karibu $20,000,000 kwa kutumia hesabu za siri za benki ya Kiswiss, kampuni hiyo ilitozwa faini ya $50,000. Lakini ilikuwa imepokea $225,000 kwa malipo ya haramu. Mwanakampuni mmoja mkuu aliapa kwa uongo katika kesi kubwa. Alitozwa faini ya $30,000 na kuhukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja. Hakukaa hata kidogo jelani.

Juma moja baadaye, karani mmoja wa usafirishaji asiyeajiriwa, mwenye mke na watoto wawili, alishtakiwa kwa kuiba televisheni. Alipokea hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja​—⁠kahukumiwa na hakimu yule yule. Kwa sababu mambo kama hayo hutokea mara nyingi sana, watu wengi huenda wakawaza hivi: “Kadiri ulivyo mkubwa, ndivyo usivyoanguka sana na ndivyo unavyotendewa kwa huruma zaidi.”

Katika nchi nyingi, uvunjaji wa sheria katika afisi unaleta hasara kubwa zaidi kuliko uvunjaji wa sheria barabarani. Shirika U. S. Chamber of Commerce linakadiri kwamba uvunjaji wa sheria wa afisini kama kuhongwa, kuchukua fedha za watu kwa siri kwa kutumia mamlaka, kupunja na kushindana kwa haramu na wizi, unaleta hasara ya karibu $42 bilioni kwa mwaka. Hata hivyo ni mara chache wenye hatia ya uvunjaji huo wa sheria wanapoadhibiwa vikali. Na sana sana hii inafanya raia wa kawaida tu watozwe kodi za juu zaidi, inafanya bei zipande zaidi na inafanya malipo ya bima yawe juu zaidi.

Huenda sheria za kulipa kodi zikapendelea matajiri. Mwaka wa 1972 karibu Waamerika 400 wenye mapato ya zaidi ya $100,000 hawakulipa kodi zo zote za serikali. Wanne kati yao walikuwa na mapato ya zaidi ya $1,000,000.

Kwa hiyo, maoni mabaya yasiyo na msingi na upendeleo kwa sababu ya cheo katika maisha, utajiri, kabila, rangi, taifa na lugha yanaleta uonezi na ubaguzi kwa mamilioni ya watu katika nchi nyingi. Wao wanadhani maisha yasiyo na udhalimu ni ndoto tu.

Hata hivyo, uko upande mwingine wa kuangalia. Nyakati nyingine wenye kupata mamlaka wanapendelea watu wachache kadha kwa sababu ya uchache wao. Inaweza kusemwa kwamba “sikuzote goigoi ndiye mwenye haki”​—⁠hata anapokuwa mwenye kosa. Hata hiyo si haki.

Na mara nyingi ni jambo gani hutukia wakati wale ambao wamebaguliwa katika nchi kwa sababu ya kabila, rangi au taifa wanapopata mamlaka katika nchi hiyo? Je! mara nyingi wao wenyewe hawaonyeshi chuki isiyo na msingi na kutopendelea wale wasio wa aina yao? Kwa njia hiyo udhalimu unaendelea, unasitawi.

Hali hiyo si mpya. Karibu miaka elfu tatu iliyopita mwandikaji wa Biblia mwenye kuongozwa na Mungu aliandika maneno haya: “Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, aliye juu kuliko walio juu huangalia; tena wako walio juu kupita hao.”​—⁠Mhu. 5:8.

Naam, mara nyingi rushwa kati ya wakuu inaonyesha kwamba walio wakubwa zaidi yao wanaipokea pia. Basi, si ajabu kwamba raia wa kawaida hunyonywa sana.

Basi, kinachohitajiwa ni nini? Watu wa aina zote wanawezaje kila mahali kuwa na maisha yasiyo na udhalimu?

JINSI “NDOTO” ITAKAVYOKUWA JAMBO HALISI

Kwa wazi, lazima jambo fulani libadilike. Kwa kweli badiliko linahitajiwa katika taratibu yote ya mambo inayofanya kazi sasa duniani. Ni badiliko kubwa kadiri gani? Je! inatosha kubadili pande fulani za taratibu hii, kufanya mabadiliko ya wakuu na ya usimamizi, au kufanya mabadiliko ya sheria fulani?

Sivyo, kinachohitajiwa hasa ni taratibu nzima ya sasa ibadilishwe na taratibu mpya yenye msingi mpya. Sisi tumeona aina zote za mabadiliko, mabadiliko ya wakuu na ya usimamizi, sheria mpya, katika nchi baada ya nyingine. Lakini, yajapokuwapo hayo, rushwa inaendelea kusitawi kati ya wakuu wa serikali. Na wakati watu mmoja mmoja wanapojaribu kuendeleza haki, mara nyingi wanashindwa kwa sababu ya kufikiria faida zao wenyewe.

Kama vile msimamizi mmoja wa chama fulani cha sheria cha Georgetown University anavyosema, “taratibu ya haki inaweza kufaa raia wakiwa na hakika tu kwamba itafaa. . . . lazima raia waamini kwamba serikali na jamii ya watu inastahili kuaminiwa, kuheshimiwa na kushikamanwa nayo kwa uaminifu.” Taratibu hiyo inaweza kutokeaje?

Kwa sababu Yehova Mungu hupenda haki, ameahidi kuleta taratibu mpya kabisa katika dunia hii ikisimamiwa na serikali ya kimbinguni. Ilitabiriwa juu ya Kristo Yesu, yeye aliyewekwa kuwa mkuu wa serikali hiyo, kwamba ‘roho ya Yehova itakaa juu yake,’ ilete hekima, ufahamu, mashauri, nguvu na maarifa, na “furaha yake itakuwa katika kumcha [Yehova].” Hiyo italetea raia zake faida gani? Unabii unaendelea kusema hivi: “Wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili.”​—⁠Isa. 11:2-4.

Alipokuwa duniani Kristo Yesu alizionyesha sifa zizi hizi atakazotumia katika utawala wake wa Ufalme juu ya dunia. Alipokuwa akiyatazama makundi ya watu yaliyokusanyika yapate kumsikia akisema, “aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji,” nalo lawama kubwa lilikuwa juu ya viongozi wa kidini wanafiki wa siku hizo kwa sababu ya watu hao kuwa katika hali hiyo. (Mt. 9:36; linganisha Mathayo 23:23, 24; Marko 12:38-40.) Alifundisha wanafunzi wake kupenda watu wote, ‘wakitoa bure kama walivyopata bure.’ (Mt. 5:43-48; 10:8) Alionyesha alikuwa na upendo wa kutojifikiria mwenyewe kwa kutoa uhai wake kwa ajili ya wanadamu wote.

‘Roho ya Yehova’ ambayo serikali ya Ufalme itakuwa nayo duniani mwote inahakikisha kabisa kwamba wote watatendewa kwa haki. Mtume mwenye kuongozwa na Mungu aliandika hivi juu Yake: “Hakika . . . Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.”​—⁠Matendo 10:34, 35.

Jipe moyo basi, na utumie wakati ujifunze katika Neno la Mungu jinsi unavyoweza kupata uzima chini ya utawala wenye haki wa Mwanawe wakati maisha yasiyo na udhalimu yatakapokuwa halisi.

[Picha katika ukurasa wa 195]

“Msitazame nafsi za watu [kwa upendeleo] katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa.”​—⁠Kum. 1:17.

“Utamhukumu jirani yako kwa haki.”​—⁠Law. 19:15.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki