Historia ya Mashahidi wa Yehova katika Nyakati za Kisasa
—Ujeremani (Inaendelea)
MACHI 1938 uandikaji wa barua wa mashahidi wa Yehova katika kambi za mateso ulipigwa marufuku. Hii iliendelea kwa miezi sita, na wakati huo akina ndugu wasingeweza kuandikia watu wao wa ukoo wala hao wasingeweza kuwaandikia waliokuwa katika kambi za mateso. Hata baada ya marufuku hiyo kuondolewa, kwa miaka mitatu na nusu au minne hivi kila mmoja wa mashahidi wa Yehova angeweza kuandikia watu wake wa ukoo mistari mitano tu, na hata katika kambi nyingine jambo hili liliendelea kwa muda mrefu zaidi. Yaliyoandikwa yalisema hivi: “Barua yenu nimeipokea; asanteni sana. Mimi mzima, mwenye afya na mchangamfu. . . . Lakini nyakati nyingine mtu alipashwa habari za kwamba atauawa kabla barua haijafika iliyosema: “Mimi mzima, mwenye afya na mchangamfu.” Katika nafasi iliyo wazi juu ya barua maandishi yafuatayo yalipigwa chapa: “Mfungwa angali Mwanafunzi wa Biblia mwenye shingo ngumu kama zamani, naye anakataa kuyaacha mafundisho ya uongo ya Wanafunzi wa Biblia. Kwa hiyo amenyimwa yale mapendeleo ya kawaida ya kuandika barua.”
“MIRABA-MINNE” AKUTANA NA WA KUMWEZA
Maisha katika kambi ya mateso yalijawa na wasiwasi wake wa kila siku, mara nyingi ukiletwa na amiri (askari) wa kambi mwenyewe. Kwa muda fulani amiri katika Sachsenhausen alikuwa mtu aliyeitwa Baranowsky, na kwa sababu ya ukubwa wake na nguvu zake nyingi wafungwa wakambandika jina la “Miraba-minne.”
Kwa kawaida yeye mwenyewe ndiye aliyekwenda kusalimu wafungwa wapya walipofika na kuwatolea ‘hotuba yake ya kuwakaribisha.’ Kwa kawaida ilianza kwa maneno haya: ‘Mimi ndimi amiri wa kambi nami naitwa “Miraba-minne.” Haya sikilizeni, nyote! Mwaweza kupata cho chote mtakacho kwangu—risasi ya kichwa, risasi ya kifua, risasi ya tumbo! Mwaweza kukata koo zenu mkitaka hata kupasua mishipa yenu ya moyo! Mwaweza kutoroka kupitia ua wenye umeme mkitaka. Nyie mkumbuke tu watu wangu hawakosei! Watawapelekeni moja kwa moja mpaka mbinguni!’ Akawa akimchezea-chezea Yehova na jina lake takatifu.
Lakini mwanzoni mwa marufuku waliyopigwa mashahidi wa Yehova kijana wa karibu miaka 23 wa Dinslaken akawa amejifunza kweli. Jina lake alikuwa August Dickmann. Hakuwa amebatizwa, Gestapo walimkamata wakamleta afanyiwe kesi. Alipomaliza kifungo chake akalemewa na Gestapo hata akatia sahihi “tangazo,” bila shaka akitumaini kwamba hii ingemwepusha na mateso zaidi. Hata hivyo, akafungwa katika Sachsenhausen Oktoba wa 1937 mara tu baada ya kumaliza kifungo chake gerezani. Akina ndugu huko wakatumia kila nafasi waendelee kuwa wenye furaha na kutiana moyo wazungumze, na kwa kuwa sasa yeye alikuwa kati yao akatambua kwamba amekubali alivyoambiwa afanye na maadui kwa sababu ya udhaifu wake. Akatubu akaomba maneno aliyotia sahihi yafutwe.
Kwa sasa ndugu yake wa kimwili Heinrich alikuwa amefungwa pia katika kambi ya Sachsenhausen. August akampasha habari alitia sahihi maneno hayo lakini akaomba yafutwe.
Juma chache zilizofuata zikapita mbio mbio. Vita ya ulimwengu ya pili ilipotokea kipindi cha mwisho cha 1939, amiri wa kambi, Baranowsky, akaanza kutimiza mipango yake. Akapata nafasi yake wakati mke wa August Dickmann alipotumia mumewe kadi yake ya jeshi, iliyokuwa imetumwa nyumbani kwao Dinslaken. Siku tatu baada ya vita kutokea, Dickmann akaagizwa aende kwenye “idara ya kisiasa.” Kabla watu wote hawajaitwa majina, Heinrich, ambaye alikuwa amekwisha pashwa habari za tukio hili jipya na August, akamwonya awe tayari kwa lo lote litakalotukia. Lazima ajue la kufanya. August kajibu: “Wanifanyie lo lote watakalo. Sitatia sahihi wala kukubaliana nao tena.”
Kesi ikafanywa alasiri hiyo, lakini August hakuwarudia akina ndugu. Ikajulikana baadaye kwamba alikuwa amekataa kutia sahihi kadi ya kuingia jeshi akatoa ushuhuda mzuri. Akafungwa akiwa peke yake katika jela ya chinichini naye amiri wa kambi akampasha Himmler mambo yalivyokuwa, akamwomba ruhusa amwue Dickmann hadharani mbele ya akina ndugu na watu wa kambi yote. Akawa na imani ya kwamba mashahidi wengi wa Yehova wangetia sahihi wakitishwa na kifo. Kufikia hapo wengi wao walikuwa wamekataa kufanya hivyo, lakini walitishwa-tishwa. Himmler akajibu kwa kumwandikia barua kwamba Dickman amehukumiwa kufa na kwamba auawe. Sasa njia ikawa wazi “Miraba-minne” ajionyeshe kweli kweli.
—Kutoka 1974 Yearbook of Jehovah’s Witnesses.