Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 11/1 kur. 3-4
  • Je! Kweli Nyakati Zetu Ni Tofauti?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kweli Nyakati Zetu Ni Tofauti?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Uchafuzi wa Mazingira
  • Idadi Kubwa Mno ya Watu
  • Silaha
  • Uchafuzi—Nani Huusababisha?
    Amkeni!—1990
  • Je! Wanadamu Wanaweza Kuleta Amani na Usalama Wenye Kudumu?
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
  • Tumefanikiwa Kadiri Gani Kuokoa Mazingira Yetu?
    Amkeni!—2003
  • Je! Sayansi Yaweza Kutatua Matatizo ya Karne ya 21?
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 11/1 kur. 3-4

Je! Kweli Nyakati Zetu Ni Tofauti?

AKIELEZA ilivyo hali ya wakati huu ya ulimwengu, mwanauchumi Mwamerika Peter F. Drucker alisema: “Hakuna mtu anayehitaji kuambiwa kwamba kipindi chetu ni kipindi cha hatari isiyo na mwisho. Hakuna mtu anayehitaji kuambiwa kwamba ulizo kubwa tunalokabili kuhusiana na wakati ujao wa mwanadamu si utakuwa nini, bali kama utakuwako.”

Ni baadhi ya matatizo gani yanayowafanya watu wengi watake kujua ikiwa wanadamu wana wakati ujao wo wote? Ni hatari gani zinazotofautisha nyakati zetu na zile za vizazi vilivyotangulia?

Uchafuzi wa Mazingira

Hewa katika miji mingi mikubwa imekuwa yenye kuhatirisha afya. Bahari, maziwa ya maji na mito inachafuliwa na takataka za viwanda, na kuambukiza samaki tunaokula. Tabaka ya anga inayolinda iitwayo ozone inaharibiwa na mivuke michafu. Kuna sababu nzuri kwamba uchafuzi wa mazingira ni jambo linalohangaikiwa na mataifa yote. Mkutano mmoja wa OECD (Tengenezo la Ushirikiano wa Kiuchumi na Usitawi) uliripotiwa katika gazeti la kila siku la Kifaransa liitwalo Le Monde: “Kuanzia 1965 mpaka 1975 mazingira yaliharibiwa vibaya sana. Hata tukitumaini kuharibika kwa uchumi kupunguze ukuzi [wa viwanda], mazingira ya asili yataendelea kuharibika katika miaka ijayo ikiwa ulinzi hautazidishwa.”

Wengine wanadai kwamba uchafuzi wa mazingira si jambo jipya. Kama hiyo ingekuwa kweli, basi mbona sanamu zilizochongwa ambazo zimekuwako kwa maelfu ya miaka ghafula zimo hatarini? “Siku baada ya siku anga lililochafuliwa la Athene linafaulu kuharibu walichoshindwa kuharibu majeshi ya Uturuki wakati walipokuwa wameitwaa Ugiriki kwa miaka 400. Polepole marmar [mawe yenye thamani] inaliwa.”​—Gazeti Le Figaro la Paris.

Idadi Kubwa Mno ya Watu

Mambo mengine yanazidi kufanya hali iwe ngumu ulimwenguni pote. Gazeti la kisayansi la kila mwezi la Ufaransa liitwalo Science et Vie (Sayansi na Uhai) lilisema hivi juu ya ukuzi wa idadi ya watu na kupanuka kwa majangwa: “Idadi ya watu wa ulimwengu huu itaongezeka kutoka bilioni nne mpaka bilioni sita kufikia mwaka 2000, nayo ardhi inayotumiwa kwa kilimo yawezekana itapunguzwa kwa asilimia 30 katika kipindi icho hicho, kwa ajili ya kukuza mazao mengi mno . . . na utengenezaji wa miji. Maelekeo hayo mawili yenye kutokea wakati mmoja yanatayarisha njia ya kutokea kwa hali isiyoongozeka hata kidogo.”

Ni kweli kwamba ukuzi wa watu umepungua katika nchi fulani za Ulaya na nchi fulani zinazofanya maendeleo. Lakini, kulingana na wataalamu, idadi kubwa mno ya watu itaendelea kuwapo mpaka angalau katikati ya karne ijayo, kwa maana katika nchi nyingi kiwango cha ukuzi kinaongezeka na kitaendelea kuongezeka. Hesabu kubwa sana ya nchi zinazoendelea ni kati ya nchi za ulimwengu zenye idadi kubwa zaidi ya watu. Idadi kubwa mno ya watu inatia alama nyakati zetu kuwa tofauti kabisa na nyakati zilizopita.

Silaha

Huenda ukawa unajua kwamba wengi wanahangaishwa sana na mashindano ya uundaji wa silaha. Mamilioni ya watu wa Ulaya wana wasiwasi juu ya kuishi mahali panapoweza kupigwa na makombora yaliyoko katika nchi za Ulaya ya Mashariki au kwa kuwa wamo mahali palipo na makombora ya Amerika. Lakini hata uwe unaishi wapi duniani kuna sababu ya kuhangaishwa na silaha zenye kuangamiza kwa miale ya nuru au silaha zenye kuangamiza kwa nguvu nyingi sana za mmweko, silaha zenye viini vinavyoua au hatari zinazotokana na masetelaiti au vituo vya angani vinavyozunguka. Zaidi ya hayo, wataalamu wengine wanaziona silaha hizo kuwa zinaamua upya ni nani mwenye kutia hofu zaidi kwa uwezo wa kijeshi. Hali ya kujisikia rahisi kushambuliwa zinayotokeza yaweza kuongoza taifa fulani lifikirie ingekuwa kwa faida yalo kushambulia kwanza.

Jiulize mwenyewe hivi: Je! vizazi vilivyotangulia vilikuwa na uwezo mkubwa hivyo wa kuharibu wakaaji wengi zaidi wa dunia katika dakika chache tu? Au je, hiyo ni hali iliyo ya pekee katika siku zetu?

Hatari kama tulizokwisha kutaja hutokeza maitikio mbalimbali, hasa katika nchi zenye usitawi wa viwanda. Raia fulani hufanya halmashauri za kupigana na uchafuzi wa mazingira; wengine wanatafuta usalama kwa vyo vyote kwa kujipatia silaha, kujenga mahandaki ya kujilinda au hata kukimbilia maeneo yaliyo peke yake. Likieleza juu ya namna hiyo ya pili ya watu, gazeti International Herald Tribune lilisema: “Vikundi vidogo lakini vyenye kukua vya Waamerika vinajipatia silaha na kujifunza jinsi ya kuua kwa sababu wamesadikishwa kwamba utaratibu wa kijamii unaharibika na kwamba watalazimika kujiangalia ili waokoke.” Watu mmoja mmoja katika nchi nyinginezo, pia, wanajizoeza kutumia silaha​—wanawake kwa wanaume.

Lakini huenda kukawa hatari ya aina nyingine ambayo ni ngumu hata zaidi kuiokoka au kushughulika nayo​—haribiko kubwa la uchumi. Kuna mamilioni ya watu wasioajiriwa kazi katika nchi za Uzunguni, nazo nchi za Ulaya ya Mashariki zina matatizo mengine ya kiuchumi. Je! wewe huoni matokeo ya mchafuko wa kiuchumi mahali unapoishi? Mwishoni-mwishoni mwa mwaka 1980 aliyekuwa waziri mkuu wa Ufaransa, Raymond Barre alisema hivi juu ya uchumi wa ulimwengu: “Ni... tisho la ulimwenguni pote. Si la muda mfupi wala si la juujuu tu, bali ni la kudumu na lenye mizizi iliyoingia ndani sana.” Mwanauchumi Samuel Pisar alisema: “Kila jambo linaonyesha na kushuhudia uhakika wa kwamba tumekaribia anguko jipya. Matatizo yetu hayafanani hata kidogo na yale ya miaka 40 iliyopita, na jambo hilo linaongeza tu woga wetu.” Kwa hiyo unaweza kugeukia wapi katika nyakati hizi zilizo tofauti sana?

Zamani sana Yesu Kristo alizungumza juu ya wakati fulani ambao ungeonyeshwa kati ya mambo mengine na “huzuni kuu ya mataifa, wasijue njia ya kutokea.” (Luka 21:25, NW) Tukiwa tunakabiliwa na matukio hayo tofauti-tofauti, ni lazima tukubali kwamba maneno yake yanaeleza juu ya nyakati zetu, nyakati ambazo ni tofauti sana na zo zote zilizotangulia. Lakini, ikiwa Yesu kweli kweli alikuwa akitaja juu ya siku zetu, hiyo ina maana gani kwetu sisi? Je! mambo hayo yote yanadokeza kwamba badiliko kubwa limekaribia? Makala ifuatayo itakusaidia ujibu hayo.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Uchafuzi wa Mazingira

Idadi Kubwa Mno ya Watu

Silaha

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki