Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 3/15 uku. 21
  • Haya Mbele, Enyi Mashahidi!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Haya Mbele, Enyi Mashahidi!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Shangwe Kama Nini Kuketi Kwenye Meza Ya Yehova!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Kwa Msaada wa Yehova, Tuliokoka Serikali za Kimabavu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Nyimbo Mpya za Ibada!
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • Kuendeleza Imani Pamoja na Mume Wangu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 3/15 uku. 21

Haya Mbele, Enyi Mashahidi!

“Muda wa mwisho wanaazimia,/​Watumishi injili kupigania./​Shetani akiwaringia,/​Nguvu Mungu awapatia.”

Hiyo ndiyo mistari yenye kuufungua wimbo namba 29 katika kile kitabu cha nyimbo cha Mashahidi wa Yehova, Mwimbieni Yehova Sifa. Uthamini wako kwa wimbo huo huenda ukaongezewa kina kwa kujua kwamba mdundo wa wimbo huo ulitungwa katika kambi ya mateso katika Ujeremani ya Nazi. Hivi majuzi, wafanya kazi wapatao 500 wa jamaa ya Betheli ya Ujeremani katika Selters walisikiliza katika ukanda wa kunasa sauti maongezi yaliyofanywa pamoja na mtungaji wimbo huo, Erich Frost, ambaye aliripoti yanayofuata:

“ ‘Haya Mbele, Enyi Mashahidi! ’​—⁠hiyo ndiyo iliyokuwa tamaa ya moyo wetu hata wakati huo, ingawa sisi tulikuwa tukifanya kazi ngumu katika kambi ya mateso. Sikuzote akili ya mtungaji nyimbo huwa ikivuma-vuma kwa midundo mbalimbali, kwa hiyo muziki wa wimbo huo ulikuwa umekuwa katika kichwa changu kwa muda mrefu. Kikundi chenye kufanyishwa kazi ngumu ambacho mimi nilikuwamo, chenye Mashahidi 40, kilikuwa kikipigishwa miguu kila siku kwa muda wa nusu saa kikienda kwenye sehemu iliyokuwa na mtambo wa kuchujia kinyesi, nje ya kambi. Asubuhi moja tulipokuwa tukienda huko, fikira ilinijia: ‘Huu ndio wakati wa kuingiza maneno fulani ya kishairi katika ule mdundo wa kimuziki, ili kwamba uweze kuimbwa.’ Na upesi ule ubeti wa kwanza ukaanza kufanyika katika akili yangu.

“Kazi yangu ilikuwa kusafirisha rundo la udongo kwa kigari-gurudumu-moja, kwa umbali wa meta zipatazo 30. Kuongea wakati wa kazi kulikatazwa kabisa. Hata hivyo, kwa kuchagua dakika iliyofaa, mimi niliuliza kwa siri ndugu mmoja mwenye kufanya kazi karibu kama alikuwa na kumbukumbu nzuri. Yeye akasema ndiyo, kwa hiyo mimi nikamkabidhi yeye wajibu wa kutunza ule ubeti wa kwanza. Baada ya muda wa saa moja, niliuliza ndugu mwingine, na baadaye wa tatu, halafu wa nne. Kila mmoja aliombwa akariri ubeti mmoja kwa moyo.

“Tuliporudi kambini jioni hiyo, hao wanne walizirudia beti zile kwa kunitajia mimi, mmoja baada ya mwingine. Hivyo, mimi ningeweza kuongeza maneno yale kwenye nukta za sauti. Wale polisi wa SS wasingalifanikiwa sana ikiwa nukta hizo za sauti ndizo peke yazo zingaliingia mikononi mwao. Lakini sasa hali ilikuwa imekuwa hatari kupita kiasi. Kama wangalininasa mimi nikiwa na maneno hayo ya kishairi, wangalininyonga. Ningeweza kufichaje wimbo huo?

“Ndugu mmoja mzee-mzee alikuwa na wajibu wa kutunza kibanda kimoja nje ya kambi ambako baadhi ya polisi wa SS waliweka sungura wao. Katika kibanda hicho, yeye alipata mahali pa kuficha johari halisi za kiroho​—⁠matoleo kamili ya Mnara wa Mlinzi na kimoja au viwili vya vitabu vya Sosaiti. Ndugu huyo alitia uhai wake mwenyewe hatarini kwa kuingiza kiharamu vitu hivyo ndani ya kambi, hivyo akatuletea sisi habari za kujifunza. Humo ndimo yeye alificha wimbo wangu. Siku moja yeye alisema: ‘Erich, wimbo wako uko safarini. Mimi nilipata mtu aliyeupeleka Switzerland kwa posta.’ Mimi nikatusha moyo kwa kuhisi vizuri.

“Akina ndugu wa Switzerland waliupeleka Brooklyn kwa posta, ukaingia mikononi mwa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova. Maneno ya kishairi niliyoyaboronga-boronga yaligeuzwa yakawa beti tatu nzuri ajabu. Mimi nilijawa na shangwe nyingi nilipoupata wimbo huo baadaye katika kile kitabu-nyimbo kilicho kipya cha Mashahidi wa Yehova.a Leo, wimbo huo ukiwa wa namba 29, ungali unachochea Mashahidi wasimame imara upande wa Yehova na ukweli! ”

[Footnotes]

a Wimbo huo uliimbwa kwa mara ya kwanza katika United States na kikundi cha wanafunzi wa darasa la 11 la Shule ya Biblia ya Gileadi ya Mnara wa Mlinzi ukiwa sehemu kubwa ya programu ya kuhitimu kwao, Agosti 1, 1948.

[Box on page 21]

Erich Frost alimaliza mwendo wake wa kidunia siku ya 0ktoba30, 1987, akiwa na umri wa 86. Akiwa amezaliwa Desemba 22, 1900, yeye alibatizwa Machi 4, 1923, na aliingia huduma ya wakati wote katika 1928. Katika 1936, yeye alitiwa katika daraka la kusimamia kazi ya chinichini ya mashahidi wanyanyaswa wa Yehova katika Ujeremani, na alitunza vizuri mgawo huo kwa miezi minane mpaka alipotiwa gerezani katika kambi ya mateso. Baada ya vita, kutoka 1945 mpaka 1955, yeye alitumikia akiwa mwangalizi wa afisi ya tawi ya Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi katika Ujeremani. (Ona Mnara wa Mlinzi [wa Kiingereza], Aprili 15, 1961, kur. 244-9.) Baada ya hapo, yeye aliendelea kutumikia Yehova kwa uaminifu. Mungu hasahau kazi ya Wakristo wapakwa-mafuta kama hao au upendo ambao wanaonyesha kwa ajili ya jina lake.​—⁠Waebrania 6:10.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki