Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 7/1 kur. 14-15
  • Kutukuza Jina la Yehova Katika Visiwa vya Bahari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutukuza Jina la Yehova Katika Visiwa vya Bahari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Vichwa vidogo
  • Yehova—Jina Lenye Kujulikana Vizuri Sana Hapo Mwanzoni
  • Majaribio ya Kukandamiza Jina Hilo
  • Mteteaji wa Jina Hilo
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 7/1 kur. 14-15

Kutukuza Jina la Yehova Katika Visiwa vya Bahari

WAZIA mshangao wa mpeleleza-nchi ambaye anapokanyaga kisiwa “kisichojulikana,” anakuta bendera ya nchi yake huko katika mahali pa wazi kabisa. Mapema katika karne ya 19, John Williams, mshiriki wa London Missionary Society, alipatwa na mshangao unaofanana na huo alipowasili katika Rarotonga, kisiwa kidogo katika Cook Islands, kusini mwa Pasifiki. Katika kisiwa hiki ambapo yeye alijifikiria kuwa ndiye mwakilishi wa kwanza wa Jumuiya ya Wakristo, aligundua madhabahu moja iliyojengwa kwa heshima ya Yehova na Yesu Kristo. Usimulizi wa safari-bahari zake za umisionari unatoa elezo linalofuata:

Miaka fulani kabla ya kuwasili kwa Williams, mwanamke mmoja alikuwa amekuja kutoka Tahiti na akanena kwa wakaaji juu ya ajabu alizokuwa ameona katika nchi yake ya kienyeji. Mwanamke huyo alisimulia juu ya kuwako kwa watu weupe wenye kuitwa Wakuki (kwa kufuatishwa na jina la Kapteni Cook). Yeye alieleza juu ya vyombo vya madini walivyovitumia badala ya mifupa ili kukata miti na kufanya mitumbwi kwa urahisi mwingi na kwa kasi Lakini yeye aliwaambia pia kwamba hao watu weupe waliabudu Mungu Yehova na Yesu Kristo. Kwa kuvuviwa upendezo hivyo, mjomba wa mfalme wa kisiwa hicho aliamua kujenga madhabahu na marae iliyowekwa wakfu kwao.a Kwa njia hii, jina la kibinafsi la Mungu liliwatangulia wamisionari wa Jumuiya ya Wakristo kwenye Visiwa vya Polinesia.

Yehova—Jina Lenye Kujulikana Vizuri Sana Hapo Mwanzoni

Wakati wao walipoanza kufundisha dini yao kwa jamii za watu wa Polinesia, wamisionari wa Jumuiya ya Wakristo waligundua kwamba miungu mingi ilikuwa ikiabudiwa katika visiwa hivyo. Ili waepuke mvurugo wo wote pamoja na miungu hii, wao walianza kurejeza kwenye Mungu Aliye Mkuu Zaidi kwa jina lake, badala ya kurejeza kwake kwa mtajo wa cheo kama vile Bwana, yule Wa-Milele, au hata Atua, ambalo ndilo neno la kusema “Mungu” katika nyingi za lugha za Kipolinesia. Hivyo wakaaji wa visiwa hivi walijifunza kupelekea Yehova sala, wakitumia jina lake la kibinafsi.

Baadaye, tafsiri za kwanza za Biblia zilitokea katika lugha za kienyeji. Kulingana na jambo lililo la kiakili kufanya, wao walitumia jina la kibinafsi la Mungu: Iehova katika Kihawaii, kirarotonga, Kitahiti, na Kiniuea; Ieova katika Kisamoa; na Ihowa katika Kimaori. Na jambo lililo la kustahili zaidi kuangaliwa ni kwamba, katika tafsiri nyingi jina hilo hata lilionekana katika Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo (Agano Jipya).

Kizazi kilicho cha zamani kidogo cha Wamaori katika New Zealand kinaweza bado kukumbuka wakati ambapo jina la Yehova lilikuwa likitumiwa sana—hasa katika marae. Katika pindi zilizo rasmi, manukuu kama vile “hofu ya Yehova ndiyo mwanzo wa hekima” yalikuwa sehemu ya hotuba ya ufunguzi yenye kukaribisha waheshimiwa wenye kuzuru. Katika sehemu zote za Polinesia, jina hilo lilitumiwa kwa uhuru kwenye ibada za kanisani. Mpaka leo hii, watu walio na umri mkubwa zaidi wana ufahamivu wa jina la Mungu katika Iugha ya kikwao. Hata hivyo, hivi sivyo ilivyo kwa habari ya kizazi cha walio wachanga zaidi, ambao waepeperuka mbali kutoka kwenye njia ya maisha ya kimapokeo.

Majaribio ya Kukandamiza Jina Hilo

Baada ya muda, hesabu fulani ya tafsiri za Kipolinesia zilisahihishwa. Sawa na vile imetukia kuhusiana na fasiri tofauti-tofauti zilizofanywa katika Ulaya na Amerika ya Kaskazini, moja la mabadiliko makuu lilikuwa kuondolewa kabisa kwa jina Yehova (au baadhi ya milingano inayokaribiana sana nalo). Hivyo, mahali palo palichukuliwa na Alii (Bwana) katika chapa iliyosahihishwa ya Biblia ya Kisamoa iliyotokea katika 1969, na fasiri inayofanana na hiyo ilipangwa kufanywa katika Kiniuea.

Ni kweli, wakaaji wa Polinesia hawaabudu tena miungu au sanamu zao kama katika wakati uliopita, wala hawaabudu hata Io wa Uso Uliofichwa, yule aliyekuwa mungu mkuu zaidi wa Wamaori. Lakini je! hiyo kwa vyo vyote inawapa watafsiri wa Biblia mamlaka ya kushusha Mungu wa Biblia awe mkosefu wa jina kwa kuweka mahali pa jina lake mtajo wa cheo tu? Je! leo jina hili limepungukiwa umaana? Kwa uhakika sivyo, kwa kuwa katika ile sala ya kiolezo, Yesu mwenyewe alifundisha wanafunzi wake kusali kwanza kabisa ili jina hilo lipate utakaso.b

Mteteaji wa Jina Hilo

Yajapokuwako matukio haya ya hivi majuzi, jina Yehova haliko karibu kutoweka katika Polinesia. Kwa nini? Kwa sababu, sawa na vile ilivyo katika mabara mengine yote, Mashahidi wa Yehova wanazuru kwa ukawaida wakaaji wa visiwa hivi ili kuwajulisha jina hilo. Sasa hivi Mashahidi zaidi ya 16,000 katika sehemu hii ya ulimwengu wanashiriki katika kazi hii ya maana, na wanaonyesha mwanadamu mwenzao umaana wa kuwa na maarifa sahihi ya kujua Neno la Mungu na kutumia maarifa hayo katika mazoea. Hiyo ndiyo maana ya kuabudu Mungu na kutakasa jina lake.​—Yohana 4:21-24.

[Maelezo ya Chini]

a Hapo kwanza marae ilikuwa kiwanja kilichozungushiwa ua ambacho kilitumiwa kwa makusudi ya kidini na ya kijamii. Leo kwa ujumla kinarejeza kwenye mahali pa mikutano ya kikabila.

b Sala ya kiolezo ambayo Yesu alifundisha wanafunzi wake (ambayo mara nyingi inaitwa Baba Yetu) inaanza kwa maneno haya: “Baba yetu katika mbingu, acha jina lako litakaswe.”​—Mathayo 6:9, NW.

[Ramani katika ukurasa wa 14]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Hawaii

Samoa

Niue

Tahiti

Rarotonga

New Zealand

[Picha katika ukurasa wa 15]

Tutuila, American Samoa

Ziwa Gunn, New Zealand

Savaii, Samoa ya Magharibi

Ufuo wa Avatele Katika Niue

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki