Biblia—Tafsiri ya Ulimwengu Mupya Habari Zenye Kuwa Katika Mwanzo MWANZO HABARI ZENYE KUWA NDANI 1 Uumbaji wa mbingu na dunia (1, 2) Siku sita za kutayarisha dunia (3-31) Siku ya 1: mwangaza; muchana na usiku (3-5) Siku ya 2: anga (6-8) Siku ya 3: inchi kavu na mimea (9-13) Siku ya 4: vitu vya kutoa mwangaza katika mbingu (14-19) Siku ya 5: samaki na ndege (20-23) Siku ya 6: wanyama wa inchi kavu na wanadamu (24-31) 2 Mungu anapumuzika siku ya saba (1-3) Yehova Mungu, Mutengenezaji wa mbingu na dunia (4) Mwanaume na mwanamuke katika bustani ya Edeni (5-25) Mutu anaumbwa kwa mavumbi (7) Muti wa ujuzi wenye ulikatazwa (15-17) Kuumbwa kwa mwanamuke (18-25) 3 Mwanzo wa zambi ya wanadamu (1-13) Uongo wa kwanza (4, 5) Yehova anahukumu waasi (14-24) Uzao wa mwanamuke unatabiriwa (15) Kufukuzwa katika Edeni (23, 24) 4 Kaini na Abeli (1-16) Wazao wa Kaini (17-24) Seti na Enoshi mwana wake (25, 26) 5 Kuanzia Adamu mupaka Noa (1-32) Adamu anazaa watoto wanaume na watoto wanamuke (4) Enoko alitembea pamoja na Mungu (21-24) 6 Wana wa Mungu wanajichukulia wanamuke katika dunia (1-3) Wanefili wanazaliwa (4) Uovu wa wanadamu unamuhuzunisha Yehova (5-8) Noa anapewa kazi ya kujenga safina (9-16) Mungu anatangaza kuja kwa Garika (17-22) 7 Kuingia ndani ya safina (1-10) Garika katika dunia yote (11-24) 8 Maji ya Garika yanapunguka (1-14) Njiwa anatumwa (8-12) Kutoka ndani ya safina (15-19) Ahadi ya Mungu juu ya dunia (20-22) 9 Maagizo kwa wanadamu wote (1-7) Sheria juu ya damu (4-6) Agano la upinde wa mvua (8-17) Unabii juu ya wazao wa Noa (18-29) 10 Oroza ya majina ya mataifa (1-32) Wazao wa Yafeti (2-5) Wazao wa Hamu (6-20) Nimrodi anamupinga Yehova (8-12) Wazao wa Shemu (21-31) 11 Munara wa Babeli (1-4) Yehova anavuruga luga (5-9) Kuanzia Shemu mupaka Abramu (10-32) Familia ya Tera (27) Abramu anahama Uru (31) 12 Abramu anahama Harani na kuenda Kanaani (1-9) Ahadi ya Mungu kwa Abramu (7) Abramu na Sarai katika inchi ya Misri (10-20) 13 Abramu anarudia Kanaani (1-4) Abramu na Loti wanatengana (5-13) Mungu anarudilia ahadi yenye alimupatia Abramu (14-18) 14 Abramu anamuokoa Loti (1-16) Melkisedeki anamubariki Abramu (17-24) 15 Agano kati ya Mungu na Abramu (1-21) Miaka mia ine ya mateso inatabiriwa (13) Mungu anarudilia ahadi yenye alimupatia Abramu (18-21) 16 Hagari na Ishmaeli (1-16) 17 Abrahamu atakuwa baba ya mataifa mengi (1-8) Abramu anapewa jina Abrahamu (5) Agano la kutahiriwa (9-14) Sarai anapewa jina Sara (15-17) Mutoto mwanaume Isaka anaahidiwa (18-27) 18 Malaika watatu wanamutembelea Abrahamu (1-8) Sara anaahidiwa kuzaa mutoto mwanaume; Sara anacheka (9-15) Abrahamu anamulilia Mungu asiharibu Sodoma (16-33) 19 Loti anatembelewa na malaika (1-11) Loti na familia yake wanaambiwa waondoke (12-22) Miji ya Sodoma na Gomora inaharibiwa (23-29) Bibi ya Loti anageuka kuwa nguzo ya chumvi (26) Loti na mabinti wake (30-38) Mwanzo wa Wamoabu na Waamoni (37, 38) 20 Sara anaokolewa katika mikono ya Abimeleki (1-18) 21 Isaka anazaliwa (1-7) Ishmaeli anamuchekelea Isaka (8, 9) Hagari na Ishmaeli wanafukuzwa (10-21) Agano kati ya Abrahamu na Abimeleki (22-34) 22 Abrahamu anaambiwa amutoe Isaka (1-19) Uzao wa Abrahamu utaleta baraka (15-18) Familia ya Rebeka (20-24) 23 Kifo cha Sara na mahali alizikwa (1-20) 24 Kumutafutia Isaka bibi (1-58) Rebeka anaenda kukutana na Isaka (59-67) 25 Abrahamu anaoa tena (1-6) Kifo cha Abrahamu (7-11) Wana wa Ishmaeli (12-18) Yakobo na Esau wanazaliwa (19-26) Esau anauzisha haki yake ya muzaliwa wa kwanza (27-34) 26 Isaka na Rebeka katika muji wa Gerari (1-11) Mungu anamuhakikishia Isaka kwamba atatimiza ahadi yake (3-5) Kugombania visima (12-25) Agano kati ya Isaka na Abimeleki (26-33) Bibi wawili Wahiti wa Esau (34, 35) 27 Yakobo anabarikiwa na Isaka (1-29) Esau anatafuta baraka lakini anakosa kutubu (30-40) Esau anamuchukia Yakobo (41-46) 28 Isaka anamutuma Yakobo Padan-aramu (1-9) Ndoto ya Yakobo kule Beteli (10-22) Mungu anamuhakikishia Yakobo kwamba atatimiza ahadi yake (13-15) 29 Yakobo anakutana na Raheli (1-14) Yakobo anamupenda sana Raheli (15-20) Yakobo anaoa Lea na Raheli (21-29) Wana ine wa Yakobo wenye walizaliwa na Lea: Rubeni, Simeoni, Lawi, na Yuda (30-35) 30 Bilha anazaa Dani na Naftali (1-8) Zilpa anazaa Gadi na Asheri (9-13) Lea anazaa Isakari na Zabuloni (14-21) Raheli anamuzaa Yosefu (22-24) Makundi ya Yakobo yanaongezeka (25-43) 31 Yakobo anaenda Kanaani kwa uficho (1-18) Labani anamufuatilia na kumufikia Yakobo (19-35) Agano kati ya Yakobo na Labani (36-55) 32 Malaika wanakutana na Yakobo (1, 2) Yakobo anajitayarisha kukutana na Esau (3-23) Yakobo anapigana mieleka na malaika (24-32) Yakobo anapewa jina Israeli (28) 33 Yakobo anakutana na Esau (1-16) Yakobo anasafiri kuenda Shekemu (17-20) 34 Dina analalwa kinguvu (1-12) Wana wa Yakobo wanatenda kwa udanganyifu (13-31) 35 Yakobo anaondoa miungu ya kigeni (1-4) Yakobo anarudia Beteli (5-15) Benyamini anazaliwa; Raheli anakufa (16-20) Wana kumi na mbili wa Israeli (21-26) Kifo cha Isaka (27-29) 36 Wazao wa Esau (1-30) Wafalme na mashehe wa Edomu (31-43) 37 Ndoto za Yosefu (1-11) Yosefu na ndugu zake wenye wivu (12-24) Yosefu anauzishwa katika utumwa (25-36) 38 Yuda na Tamari (1-30) 39 Yosefu katika nyumba ya Potifa (1-6) Yosefu anakataa kulala na bibi ya Potifa (7-20) Yosefu katika gereza (21-23) 40 Yosefu anafasiria maana ya ndoto za wafungwa (1-19) ‘Mafasirio yanatoka kwa Mungu’ (8) Karamu ya siku ya kuzaliwa kwa Farao (20-23) 41 Yosefu anafasiria maana ya ndoto za Farao (1-36) Yosefu anainuliwa na Farao (37-46a) Yosefu anasimamia chakula (46b-57) 42 Ndugu za Yosefu wanaenda Misri (1-4) Yosefu anakutana na ndugu zake na anawajaribu (5-25) Ndugu zake wanarudia nyumbani kwa Yakobo (26-38) 43 Ndugu za Yosefu wanarudia Misri mara ya pili; pamoja na Benyamini (1-14) Yosefu anakutana tena na ndugu zake (15-23) Yosefu anafanya karamu pamoja na ndugu zake (24-34) 44 Kikombe cha feza cha Yosefu kinapatikana katika mufuko wa Benyamini (1-17) Yuda anaomba kwa kulia ili Benyamini aachiliwe (18-34) 45 Yosefu anajitambulisha (1-15) Ndugu za Yosefu wanaenda kumuchukua Yakobo (16-28) 46 Yakobo na watu wa nyumba yake wanahamia Misri (1-7) Majina ya wenye walihamia Misri (8-27) Yosefu na Yakobo wanakutana Gosheni (28-34) 47 Yakobo anakutana na Farao (1-12) Usimamizi wenye hekima wa Yosefu (13-26) Israeli anafanya makao yake kule Gosheni (27-31) 48 Yakobo anabariki wana wawili wa Yosefu (1-12) Efraimu anapata baraka kubwa zaidi (13-22) 49 Unabii wenye Yakobo alitoa akiwa kwenye kitanda wakati alikaribia kufa (1-28) Shilo atatokea katika Yuda (10) Maagizo ya kumuzika Yakobo (29-32) Kifo cha Yakobo (33) 50 Yosefu anamuzika Yakobo katika inchi ya Kanaani (1-14) Yosefu anahakikishia ndugu zake kwamba amewasamehe (15-21) Siku za mwisho za Yosefu na kifo chake (22-26) Maagizo ya Yosefu kuhusu mifupa yake (25)