Biblia—Tafsiri ya Ulimwengu Mupya Habari Zenye Kuwa Katika Yoshua YOSHUA HABARI ZENYE KUWA NDANI 1 Yehova anamutia Yoshua moyo (1-9) Soma Sheria kwa sauti ya chini (8) Matayarisho ya kuvuka Yordani (10-18) 2 Yoshua anatuma wapelelezi wawili Yeriko (1-3) Rahabu anaficha wapelelezi (4-7) Rahabu anapewa ahadi (8-21a) Alama ya kamba ya rangi nyekundu yenye kungaa (18) Wapelelezi wanarudia kwa Yoshua (21b-24) 3 Israeli wanavuka Yordani (1-17) 4 Majiwe ya ukumbusho (1-24) 5 Waisraeli wanatahiriwa kule Gilgali (1-9) Sikukuu ya Pasaka; mana inaacha kuanguka (10-12) Mukubwa wa jeshi la Yehova (13-15) 6 Ukuta wa Yeriko unaanguka (1-21) Rahabu na familia yake wanaokolewa (22-27) 7 Israeli wanashindwa kule Ai (1-5) Sala ya Yoshua (6-9) Zambi inafanya Israeli washindwe (10-15) Zambi ya Akani inafunuliwa na Akani anapigwa majiwe (16-26) 8 Yoshua anaweka watu wa kuvizia Ai (1-13) Muji wa Ai unakamatwa (14-29) Sheria inasomwa kwenye Mulima Ebali (30-35) 9 Wagibeoni wajanja wanatafuta amani (1-15) Ujanja wa Wagibeoni unafunuliwa (16-21) Wagibeoni wanakuwa watumwa wa kukusanya kuni na kushota maji (22-27) 10 Israeli wanasaidia Wagibeoni (1-7) Yehova anapigania Israeli (8-15) Mvua ya majiwe inanyeshea maadui wenye kukimbia (11) Jua linasimama bila kutikisika (12-14) Wafalme tano wenye kushambulia wanauawa (16-28) Miji ya eneo la kusini inakamatwa (29-43) 11 Miji ya eneo la kaskazini inakamatwa (1-15) Habari fupi juu ya ushindi wa Yoshua (16-23) 12 Wafalme wa eneo la mashariki mwa Yordani wanashindwa (1-6) Wafalme wa eneo la mangaribi mwa Yordani wanashindwa (7-24) 13 Maeneo yenye hayajakamatwa (1-7) Kugawanywa kwa maeneo ya mashariki mwa Yordani (8-14) Uriti wa Warubeni (15-23) Uriti wa Wagadi (24-28) Uriti wa kabila la Manase upande wa mashariki (29-32) Yehova ndiye uriti wa Walawi (33) 14 Kugawanywa kwa maeneo ya mangaribi mwa Yordani (1-5) Kalebu anariti Hebroni (6-15) 15 Uriti wa kabila la Yuda (1-12) Binti ya Kalebu anapewa eneo (13-19) Miji ya Yuda (20-63) 16 Uriti wa wazao wa Yosefu (1-4) Uriti wa kabila la Efraimu (5-10) 17 Uriti wa kabila la Manase upande wa mangaribi (1-13) Maeneo zaidi kwa ajili ya wazao wa Yosefu (14-18) 18 Maeneo yenye yalibakia yanagawanywa kule Shilo (1-10) Uriti wa kabila la Benyamini (11-28) 19 Uriti wa kabila la Simeoni (1-9) Uriti wa kabila la Zabuloni (10-16) Uriti wa kabila la Isakari (17-23) Uriti wa kabila la Asheri (24-31) Uriti wa kabila la Naftali (32-39) Uriti wa kabila la Dani (40-48) Uriti wa Yoshua (49-51) 20 Miji ya makimbilio (1-9) 21 Miji ya Walawi (1-42) Ya wazao wa Haruni (9-19) Ya Wakohati wenye walibakia (20-26) Ya Wagershoni (27-33) Ya Wamerari (34-40) Ahadi za Yehova zinatimia (43-45) 22 Makabila ya mashariki yanarudia kwao (1-8) Mazabahu inajengwa karibu na Yordani (9-12) Kusudi la mazabahu linaelezwa (13-29) Hali ya kukosa kuelewana inaisha (30-34) 23 Maneno ya Yoshua ya kuaga viongozi wa Israeli (1-16) Hakuna neno la Yehova lenye halikutimia (14) 24 Yoshua anakumbusha Israeli historia yao (1-13) Anatia watu moyo wamutumikie Yehova (14-24) “Mimi na nyumba yangu, tutamutumikia Yehova” (15) Yoshua anafanya agano na Israeli (25-28) Yoshua anakufa na anazikwa (29-31) Mifupa ya Yosefu inazikwa Shekemu (32) Eleazari anakufa na anazikwa (33)