WIMBO 50
Sala Yangu ya Kujitoa kwa Mungu
Maandishi
1. Nakupa moyo wangu
Ili nipende kweli.
Pia sauti yangu
Ikuimbie Bwana.
2. Baba nakupatia
Nguvu na mali yangu.
Pia mikono yangu
Ifanye kazi yako.
3. Yehova ninatoa
Maisha yangu yote;
Baba unikubali,
Nitakutumikia.
(Ona pia Zb. 40:8; Yoh. 8:29; 2 Ko. 10:5.)