WIMBO 28
Rafiki ya Yehova Ni Nani?
Maandishi
	- 1. Ni nani rafiki - yako eh Yehova? - Nani anakujua weye? - Nani unapenda? - Mwenye anasoma - Neno yako sana, - Mushikamanifu, na mwenye - haki na imani. 
- 2. Nani anaweza - kukukaribia? - Nani unajua kwa jina - na kufurahia? - Mwenye kukusifu - na kukusikia, - Muaminifu tena mwenye - anasema kweli. 
- 3. Tunaufungua - moyo wetu kwako, - Unatuhangaikiaka - na unatupenda. - Tunapenda sana - kukukaribia. - Hatuna rafiki mwingine - kama weye Baba. 
(Ona pia Zb. 139:1; 1 Pe. 5:6, 7.)