WIMBO 31
Utembee Pamoja na Mungu!
Maandishi
	(Mika 6:8)
- 1. Utembee kwa kiasi - Pamoja na Yehova. - Tena ukuwe muaminifu, - Na umutegemee. - Na ukitii Neno yake - Hautaanguka. - Yeye atakuongoza - Ukimusikiliza. 
- 2. Utembee kwa usafi - Pamoja na Yehova. - Hata upate jaribu gani - Atakusaidia. - Mambo ya kweli na ya haki, - na ya kusifiwa; - Uifikirie sana - Ili ubarikiwe. 
- 3. Utembee kwa furaha - Pamoja na Yehova. - Umushukuru kwa wema wake - na kwa upendo wake. - Tembea pamoja na Mungu; - Imba kwa furaha. - Na watu wote wajue, - Kama ni Mungu wako. 
(Ona pia Mwa. 5:24; 6:9; Flp. 4:8; 1 Ti. 6:6-8.)