-
Mambo ya Walawi 8:28Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
28 Kisha Musa akavichukua kutoka mikononi mwao na kuviteketeza kwenye madhabahu juu ya dhabihu ya kuteketezwa ili vifuke moshi. Vitu hivyo vilikuwa dhabihu ya kuwaweka rasmi makuhani, dhabihu yenye harufu ya kupendeza.* Vilikuwa dhabihu kwa Yehova inayochomwa kwa moto.
-
-
Hesabu 6:13Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
13 “‘Hii ndiyo sheria inayomhusu Mnadhiri: Atakapomaliza siku zake za kuwa Mnadhiri,+ ataletwa kwenye mlango wa hema la mkutano.
-
-
Hesabu 6:19Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
19 Kisha kuhani atachukua mguu wa mbele uliochemshwa+ wa yule kondoo dume, mkate mmoja wa mviringo usio na chachu kutoka katika kile kikapu, na mkate mmoja mwembamba usio na chachu, na kuviweka mikononi mwa Mnadhiri huyo baada ya nywele zake za Unadhiri kunyolewa.
-