Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 29:13
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 13 Kisha chukua mafuta yote+ yanayofunika matumbo, mafuta yaliyo juu ya ini, na figo zake mbili na mafuta yaliyo juu yake, nawe uchome moto vitu hivyo ili vifuke moshi juu ya madhabahu.+

  • Mambo ya Walawi 7:23-25
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 23 “Waambie Waisraeli, ‘Hampaswi kula mafuta yoyote+ ya ng’ombe dume au ya mwanakondoo dume au ya mbuzi. 24 Mafuta ya mnyama aliyepatikana amekufa na mafuta ya mnyama aliyeuawa na mnyama mwingine, yanaweza kutumiwa kwa kusudi lingine lolote, lakini hampaswi kamwe kuyala.+ 25 Kwa maana mtu yeyote anayekula mafuta ya mnyama anayemtoa kuwa dhabihu kwa Yehova inayochomwa kwa moto, ni lazima auawe.

  • 1 Wafalme 8:64
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 64 Siku hiyo ilimbidi mfalme atakase sehemu ya katikati ya ua ulio mbele ya nyumba ya Yehova, kwa sababu alipaswa kutolea mahali hapo dhabihu za kuteketezwa, matoleo ya nafaka, na vipande vya mafuta vya dhabihu za ushirika, kwa sababu madhabahu ya shaba+ iliyo mbele za Yehova ilikuwa ndogo sana isiweze kutoshea dhabihu za kuteketezwa, matoleo ya nafaka, na vipande vya mafuta+ vya dhabihu za ushirika.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki