-
Waamuzi 16:9Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
9 Nao wakawaficha watu fulani katika chumba cha ndani ili wamvizie, basi Delila akamwambia, “Wafilisti wamekuja kukushambulia, Samsoni!” Ndipo akazikata hizo kamba kwa urahisi kama uzi wa kitani unavyokatika unapoguswa na moto.+ Nao hawakujua siri ya nguvu zake.
-
-
Waamuzi 16:12Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
12 Basi Delila akachukua kamba mpya akamfunga nazo, kisha akamwambia hivi Samsoni kwa sauti kubwa: “Wafilisti wamekuja kukushambulia, Samsoni!” (Wakati huo watu waliokuwa wakimvizia walikuwa wamejificha katika chumba cha ndani.) Ndipo akazikata kamba hizo kutoka mikononi mwake kama nyuzi.+
-