-
Mambo ya Walawi 11:23, 24Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
23 Wadudu wengine wote wenye mabawa wanaoishi katika makundi makubwa wenye miguu minne ni chukizo kwenu. 24 Wadudu hao watawafanya msiwe safi. Kila mtu anayegusa mizoga yao hatakuwa safi mpaka jioni.+
-
-
Mambo ya Walawi 15:4, 5Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
4 “‘Kitanda chochote anacholalia mtu anayetokwa na umajimaji hakitakuwa safi, na kitu chochote anachokalia hakitakuwa safi. 5 Mtu anayegusa kitanda cha mtu huyo ni lazima afue mavazi yake na kuoga kwenye maji, naye hatakuwa safi mpaka jioni.+
-
-
Mambo ya Walawi 15:16Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
16 “‘Mwanamume akitokwa na shahawa, anapaswa kuoga mwili mzima kwenye maji naye hatakuwa safi mpaka jioni.+
-
-
Mambo ya Walawi 15:18Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
18 “‘Mwanamume akilala na mwanamke kisha atokwe na shahawa, wote wawili wanapaswa kuoga kwenye maji na hawatakuwa safi mpaka jioni.+
-
-
Hesabu 19:16Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
16 Kila mtu aliye uwanjani anayemgusa mtu aliyeuawa kwa upanga au maiti au mfupa wa mtu au kaburi hatakuwa safi kwa siku saba.+
-