-
2 Wafalme 9:24Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
24 Yehu akachukua upinde wake na kumpiga mshale Yehoramu katikati ya mabega, na mshale huo ukatokea moyoni mwake, naye akaanguka ndani ya gari lake la vita.
-
-
2 Wafalme 10:6, 7Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
6 Ndipo Yehu akawaandikia barua ya pili, akisema: “Ikiwa mko upande wangu na mko tayari kunitii, leteni vichwa vya wana wa bwana wenu na mje kwangu kesho wakati kama huu kule Yezreeli.”
Wana 70 wa mfalme walikuwa pamoja na wanaume mashuhuri wa jiji waliokuwa wakiwalea. 7 Mara tu barua hiyo ilipowafikia, wakawachukua wana wa mfalme, wanaume 70,+ na kuwachinja, kisha wakaweka vichwa vyao ndani ya vikapu, wakampelekea kule Yezreeli.
-
-
2 Wafalme 10:23Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
23 Halafu Yehu na Yehonadabu+ mwana wa Rekabu wakaingia katika nyumba ya Baali. Yehu akawaambia waabudu wa Baali: “Tafuteni kwa uangalifu mhakikishe kwamba hakuna mwabudu yeyote wa Yehova humu ndani isipokuwa waabudu wa Baali.”
-
-
2 Wafalme 10:25Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
25 Mara tu alipomaliza kutoa dhabihu ya kuteketezwa, Yehu akawaambia hivi walinzi* na makamanda wasaidizi: “Ingieni ndani na kuwaua! Msimwache yeyote aponyoke!”+ Basi walinzi na makamanda wasaidizi wakawaua kwa upanga na kuwatupa nje, wakaingia mpaka kwenye chumba kitakatifu cha ndani cha* nyumba hiyo ya Baali.
-