11 Lakini nchi mnayokaribia kuvuka kuingia humo ili kuimiliki ni nchi yenye milima na mabonde tambarare.+ Inanyweshwa na maji ya mvua kutoka mbinguni;+ 12 ni nchi inayotunzwa na Yehova Mungu wenu. Macho ya Yehova Mungu wenu yanaitazama daima, kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka.