-
1 Samweli 23:26-28Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
26 Sauli alipofika upande mmoja wa mlima, Daudi na wanaume wake walikuwa upande wa pili wa mlima huo. Daudi alikuwa akifanya haraka kumkimbia+ Sauli, lakini Sauli na wanaume wake walikuwa wakimkaribia Daudi na wanaume wake ili wawakamate.+ 27 Lakini mjumbe fulani akaja kwa Sauli na kumwambia: “Njoo haraka, kwa sababu Wafilisti wameivamia nchi!” 28 Ndipo Sauli akaacha kumfuatia Daudi,+ akaenda kukabiliana na Wafilisti. Ndiyo sababu mahali hapo paliitwa Mwamba wa Migawanyiko.
-
-
2 Samweli 17:21, 22Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
21 Baada ya wanaume hao kwenda zao, walitoka kisimani na kwenda kumjulisha Mfalme Daudi. Wakamwambia: “Ondoka, uvuke haraka maji haya, kwa maana Ahithofeli ametoa ushauri dhidi yako.”+ 22 Mara moja Daudi na watu wote waliokuwa pamoja naye wakaondoka na kuvuka Yordani. Wakati wa mapambazuko, hapakuwa na mtu hata mmoja ambaye hakuwa amevuka Yordani.
-