-
2 Samweli 22:32-43Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
32 Kwa maana ni nani aliye Mungu ila Yehova?+
Na ni nani aliye mwamba isipokuwa Mungu wetu?+
34 Huifanya miguu yangu iwe kama ya paa;
Hunifanya nisimame mahali palipo juu.+
35 Huizoeza mikono yangu kupigana vita;
Mikono yangu inaweza kuukunja upinde wa shaba.
36 Wewe hunipa ngao yako ya wokovu,
Na unyenyekevu wako hunifanya niwe mkuu.+
38 Nitawafuatia maadui wangu na kuwaangamiza;
Sitarudi mpaka watakapoangamizwa kabisa.
39 Nami nitawaangamiza kabisa na kuwaponda, hivi kwamba hawatainuka;+
Wataanguka chini ya miguu yangu.
43 Nitawaponda wawe laini kama mavumbi ya dunia;
Nitawapondaponda na kuwakanyaga-kanyaga kama matope barabarani.
-