-
Mwanzo 1:9Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
9 Kisha Mungu akasema: “Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, na nchi kavu itokee.”+ Na ikawa hivyo.
-
-
Ayubu 38:11Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
11 Nami nikaiambia, ‘Unaweza kufika hapa, lakini usipite hapa;
Hapa ndipo mawimbi yako ya kifahari yatakapokomea’?+
-
-
Zaburi 136:6Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
6 Aliitandaza dunia juu ya maji,+
Kwa maana upendo wake mshikamanifu unadumu milele.
-
-
Yeremia 5:22Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
22 ‘Je, hamniogopi mimi?’ asema Yehova,
‘Je, hampaswi kutetemeka mbele zangu?
Mimi ndiye niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari,
Sheria inayodumu isiyoweza kukiukwa na bahari.
Ingawa mawimbi yake yanasukasuka, hayawezi kushinda;
Ingawa yananguruma, bado hayawezi kuvuka.+
-