-
Danieli 4:30-32Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
30 Mfalme alikuwa akisema: “Je, hii si Babiloni Kubwa ambayo nimeijenga mimi mwenyewe kuwa makao ya kifalme kwa nguvu zangu mwenyewe na uwezo wangu na kwa ajili ya utukufu wa ukuu wangu?”
31 Mfalme alipokuwa akiendelea kusema maneno hayo, sauti ikasema hivi kutoka mbinguni: “Unaambiwa hivi, Ee Mfalme Nebukadneza, ‘Ufalme umekuponyoka,+ 32 nawe unafukuzwa mbali kutoka kati ya wanadamu. Utaishi na wanyama wa mwituni, nawe utapewa majani ule kama ng’ombe dume, na nyakati saba zitapita, mpaka utakapojua kwamba Aliye Juu Zaidi ni Mtawala katika ufalme wa wanadamu na yeye humpa ufalme huo yeyote anayetaka kumpa.’”+
-