-
Yeremia 34:15, 16Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
15 Na hivi karibuni* ninyi wenyewe mligeuka na kufanya yaliyo sawa machoni pangu kwa kuwatangazia uhuru wenzenu, nanyi mkafanya agano mbele zangu katika nyumba inayoitwa kwa jina langu. 16 Lakini mligeuka tena na kulichafua jina langu+ kwa kuwarudisha watumwa wenu wa kiume na wa kike ambao mlikuwa mmewaachilia huru kama walivyotaka, nanyi mkawalazimisha tena kuwa watumwa.’
-