-
Isaya 9:5Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
5 Kila kiatu cha askari kinachotikisa dunia kinapopiga mwendo
Na kila vazi lililoloweshwa katika damu
Litakuwa kuni kwa ajili ya moto.
-
-
Isaya 30:27Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
27 Tazama! Jina la Yehova linakuja kutoka mbali sana,
Likiwaka kwa hasira yake na kwa mawingu mazito.
Midomo yake imejaa ghadhabu,
Na ulimi wake ni kama moto unaoteketeza.+
-
-
Isaya 31:8, 9Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
8 Na Mwashuru atauawa kwa upanga, lakini si wa mwanadamu;+
Na upanga, usio wa mwanadamu, utamwangamiza.
Atakimbia kwa sababu ya upanga,
Na wanaume wake vijana watalazimishwa kufanya kazi za kulazimishwa.
9 Jabali lake litapitilia mbali kwa sababu ya woga mwingi,
Na wakuu wake wataogopa kwa sababu ya nguzo ya ishara,” asema Yehova,
Ambaye nuru yake iko* Sayuni na ambaye tanuru lake liko Yerusalemu.
-