-
Yeremia 8:18, 19Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
18 Huzuni yangu haiwezi kuponywa;
Moyo wangu ni mgonjwa.
19 Kutoka nchi ya mbali kuna kilio cha kuomba msaada
Kutoka kwa binti ya watu wangu:
“Je, Yehova hayuko Sayuni?
Au je, mfalme wake hayuko ndani yake?”
“Kwa nini wamenikasirisha kwa sanamu zao za kuchongwa,
Kwa miungu yao ya kigeni ya ubatili?”
-
-
Yeremia 9:1Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
9 Laiti kichwa changu kingekuwa maji,
Na macho yangu chemchemi ya machozi!+
Ndipo ningelia usiku na mchana
Kwa ajili ya watu wangu waliouawa.
-