-
Yeremia 27:5-7Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
5 ‘Mimi ndiye niliyeiumba dunia, wanadamu, na wanyama walio duniani kwa nguvu zangu kuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa; nami nimempa yeyote ninayetaka.*+ 6 Na sasa mimi mwenyewe nimezitia nchi hizi zote mikononi mwa mtumishi wangu Mfalme Nebukadneza+ wa Babiloni; nimempa hata wanyama wa mwituni ili wamtumikie. 7 Mataifa yote yatamtumikia yeye na mwanawe na mjukuu wake mpaka wakati wa nchi yake utakapofika,+ wakati ambapo mataifa mengi na wafalme wakuu watamfanya kuwa mtumwa wao.’+
-