-
Luka 13:25-27Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
25 Mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, mtakuwa nje mkibisha mlangoni, mkisema, ‘Bwana, tufungulie.’+ Lakini atawajibu: ‘Sijui mnatoka wapi.’ 26 Kisha mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, nawe ulifundisha katika barabara zetu kuu.’+ 27 Lakini atawaambia, ‘Sijui mnatoka wapi. Ondokeni kwangu, ninyi nyote watenda maovu!’
-