-
Marko 9:17-29Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
17 Mtu mmoja katika umati akamjibu: “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako kwa sababu ana roho anayemfanya awe bubu.+ 18 Kila mara anapomshambulia humwangusha chini, naye hutoa povu mdomoni na kusaga meno yake na kuishiwa nguvu. Niliwaambia wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.” 19 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa.”+ 20 Basi wakamleta yule mvulana kwa Yesu, lakini yule roho mwovu alipomwona, mara moja akamfanya yule mtoto agaegae. Baada ya kuanguka chini, akaendelea kujiviringisha, akitoa povu mdomoni. 21 Yesu akamuuliza baba yake: “Jambo hili limekuwa likitokea kwa muda gani?” Akasema: “Tangu utotoni, 22 naye humwangusha ndani ya moto na ndani ya maji ili amuue. Lakini ikiwa unaweza kufanya chochote, tuhurumie na utusaidie.” 23 Yesu akamwambia: “Maneno hayo, ‘Ikiwa unaweza’! Mambo yote yanawezekana kwa mtu mwenye imani.”+ 24 Mara moja baba ya yule mtoto akasema kwa sauti kubwa: “Nina imani! Nisaidie mahali ambapo ninahitaji imani!”+
25 Yesu alipoona umati ukikusanyika haraka, akamkemea yule roho mwovu, akamwambia: “Wewe roho bubu na kiziwi, ninakuagiza umtoke mtoto huyu na usimwingie tena!”+ 26 Baada ya kupaza sauti na kugaagaa sana, roho huyo akamtoka, na yule mtoto akaonekana ni kama amekufa, hivi kwamba watu wengi wakasema: “Amekufa!” 27 Lakini Yesu akamshika mkono na kumwinua, naye akasimama. 28 Baada ya kuingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza faraghani: “Kwa nini tulishindwa kumfukuza?”+ 29 Akawaambia: “Roho wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.”
-
-
Luka 9:38-42Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
38 Na tazama! mtu fulani katika umati akasema kwa sauti kubwa: “Mwalimu, ninakuomba umwangalie mwanangu, kwa sababu yeye ni mwanangu wa pekee.+ 39 Tazama! roho mwovu humshika, naye hupiga kelele ghafla, na humfanya agaegae na kutokwa na povu mdomoni, naye hamtoki upesi mpaka anapomjeruhi. 40 Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini wakashindwa.” 41 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani na kilichopotoka,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”+ 42 Lakini alipokuwa akikaribia, yule roho mwovu akamwangusha na kumfanya agaegae sana. Hata hivyo, Yesu akamkemea yule roho mwovu na kumponya mvulana huyo, kisha akamkabidhi kwa baba yake.
-