Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 14:43-47
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 43 Na mara moja, alipokuwa bado akizungumza, Yuda, mmoja wa wale 12, akafika pamoja na umati wenye mapanga na marungu, walikuwa wametumwa na wakuu wa makuhani, waandishi, na wazee.+ 44 Basi msaliti wake alikuwa amewapa ishara waliyokubaliana akisema: “Yule nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni na kuondoka naye akiwa chini ya ulinzi.” 45 Akaja moja kwa moja akamkaribia na kusema, “Rabi!” kisha akambusu kwa wororo. 46 Basi wakamkamata na kumtia nguvuni. 47 Hata hivyo, mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo akauchomoa upanga wake, akampiga mtumwa wa kuhani mkuu na kumkata sikio.+

  • Luka 22:47-51
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 47 Alipokuwa bado akizungumza, tazama! umati ukaja ukiongozwa na Yuda, mmoja wa wale 12, naye akamkaribia Yesu ili ambusu.+ 48 Lakini Yesu akamuuliza: “Yuda, unamsaliti Mwana wa binadamu kwa busu?” 49 Wale waliomzunguka walipoona jambo lililokuwa karibu kutukia, wakasema: “Bwana, tuwashambulie kwa upanga?” 50 Mmoja wao hata akampiga mtumwa wa kuhani mkuu na kumkata sikio la kulia.+ 51 Lakini Yesu akasema: “Inatosha.” Akaligusa sikio la yule mtumwa akamponya.

  • Yohana 18:3
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 3 Basi Yuda akaja na kikosi cha wanajeshi, maofisa wa wakuu wa makuhani na wa Mafarisayo, wakafika hapo wakiwa na mienge, taa, na silaha.+

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki