-
Mathayo 14:24-33Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
24 Kufikia sasa mashua ilikuwa mamia ya mita* kutoka kwenye nchi kavu, ikitaabishwa na mawimbi kwa sababu upepo ulikuwa ukivuma kinyume chao. 25 Lakini katika kesha la nne la usiku* akawajia, akitembea juu ya bahari. 26 Wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, wakahangaika na kusema: “Ni mzuka!” Wakapaza sauti kwa hofu. 27 Lakini mara moja Yesu akawaambia: “Jipeni moyo! Ni mimi; msiogope.”+ 28 Petro akamjibu: “Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako nikitembea juu ya maji.” 29 Akamwambia: “Njoo!” Ndipo Petro akatoka kwenye mashua, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30 Lakini alipoitazama ile dhoruba ya upepo akaogopa. Alipoanza kuzama, akapaza sauti: “Bwana, niokoe!” 31 Mara moja Yesu akaunyoosha mkono wake, akamshika na kumwambia: “Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini umekuwa na shaka?”+ 32 Walipopanda kwenye mashua, ile dhoruba ikatulia. 33 Ndipo wale waliokuwa ndani ya mashua wakamsujudia* wakisema: “Kwa kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”
-