-
Marko 1:23-28Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
23 Wakati huohuo, kulikuwa na mtu katika sinagogi lao aliyekuwa na roho mwovu, naye akasema kwa sauti kubwa: 24 “Kwa nini unatusumbua, wewe Yesu Mnazareti?+ Je, umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani, Mtakatifu wa Mungu!”+ 25 Lakini Yesu akamkemea, akisema: “Nyamaza, na umtoke!” 26 Na yule roho mwovu, baada ya kumfanya mtu huyo agaegae na kupiga kelele kwa sauti kubwa, akamtoka. 27 Basi, watu wote wakashangaa sana na kuulizana: “Ni jambo gani hili? Ni fundisho jipya! Hata anawaamuru roho waovu kwa mamlaka, nao wanamtii!” 28 Basi habari kumhusu zikaenea upesi kila mahali katika eneo lote la Galilaya.
-