Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 12:9-14
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 9 Baada ya kutoka hapo, akaingia ndani ya sinagogi lao, 10 na tazama! kulikuwa na mtu aliyepooza mkono!+ Basi, ili wapate sababu ya kumshtaki wakamuuliza, “Je, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato?”+ 11 Akawaambia: “Ukiwa na kondoo mmoja, naye kondoo huyo atumbukie shimoni siku ya Sabato, je, kuna yeyote kati yenu ambaye hatamshika na kumtoa humo?+ 12 Kwa kweli, mwanadamu ni mwenye thamani sana kuliko kondoo! Basi ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” 13 Kisha akamwambia mtu huyo: “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa mzima kama ule mkono mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakaenda nje na kupanga njama ili wamuue.

  • Marko 3:1-6
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 3 Yesu akaingia tena ndani ya sinagogi, na palikuwa na mtu aliyepooza mkono.+ 2 Basi walikuwa wakimwangalia sana waone kama atamponya mtu huyo siku ya Sabato, ili wamshtaki. 3 Akamwambia yule mtu aliyepooza mkono: “Simama uje hapa katikati.” 4 Kisha akawauliza: “Je, ni halali kufanya mema au kufanya mabaya siku ya Sabato, kuokoa uhai* au kuua?”+ Lakini wakanyamaza. 5 Akawatazama kwa hasira na kuhuzunika sana kwa sababu mioyo yao ilikuwa migumu,+ akamwambia mtu huyo: “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha mkono wake, nao ukapona. 6 Ndipo Mafarisayo wakaenda nje na mara moja wakafanya mkutano pamoja na wafuasi wa chama cha Herode+ ili wamuue Yesu.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki