-
Kumbukumbu la Torati 15:7, 8Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
7 “Ikiwa mmoja wa ndugu zenu atakuwa maskini miongoni mwenu katika mojawapo ya majiji yaliyo katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa, msiifanye mioyo yenu iwe migumu au kumfumbia mkono ndugu yenu maskini.+ 8 Kwa maana mnapaswa kumfumbulia mkono wenu kwa ukarimu+ na kufanya yote mwezayo kumkopesha* chochote anachohitaji au alichopungukiwa.
-
-
Methali 21:26Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
26 Anatamani kwa pupa mchana kutwa,
Lakini mwadilifu hutoa, hawanyimi wengine chochote.+
-