10 Hili ndilo agano langu nililofanya pamoja nawe, ambalo wewe na uzao wako* baada yako mtalishika: Kila mwanamume miongoni mwenu ni lazima atahiriwe.+
12 Katika vizazi vyenu vyote, kila mwanamume miongoni mwenu mwenye umri wa siku nane ni lazima atahiriwe,+ yeyote anayezaliwa nyumbani mwenu na yeyote ambaye si mmoja wa uzao wenu* na yeyote aliyenunuliwa kwa pesa kutoka kwa mgeni.
2 “Waambie Waisraeli, ‘Mwanamke akipata mimba na kuzaa mtoto wa kiume, mwanamke huyo hatakuwa safi kwa siku saba, atakuwa kama anavyokuwa katika siku zake za hedhi.+3 Siku ya nane, mtoto huyo atatahiriwa.+