-
Danieli 3:23-25Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
23 Lakini wanaume hao watatu, Shadraki, Meshaki, na Abednego, wakaanguka ndani ya tanuru hilo lenye moto mkali wakiwa wamefungwa.
24 Ndipo Mfalme Nebukadneza akaogopa, akainuka haraka na kuwauliza maofisa wake wakuu: “Je, hatukuwafunga wanaume watatu na kuwatupa ndani ya moto?” Wakamjibu mfalme: “Naam, Ee mfalme.” 25 Mfalme akasema: “Tazama! Naona wanaume wanne wakitembeatembea katikati ya moto wakiwa huru, nao hawajapatwa na madhara, na yule wa nne anaonekana kama mwana wa miungu.”
-