Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 17
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mwanzo—Yaliyomo

      • Abrahamu atakuwa baba wa mataifa mengi (1-8)

        • Abramu apewa jina jipya, Abrahamu (5)

      • Agano la kutahiri (9-14)

      • Sarai apewa jina jipya, Sara (15-17)

      • Aahidiwa kumzaa mwana aitwaye Isaka (18-27)

Mwanzo 17:1

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “bila lawama.”

Mwanzo 17:2

Marejeo

  • +Mwa 15:18; Zb 105:8-11
  • +Mwa 22:17; Kum 1:10; Ebr 11:11, 12

Mwanzo 17:4

Marejeo

  • +Zb 105:9-11
  • +Mwa 13:16; Ro 4:17

Mwanzo 17:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Maana yake “Baba Yuko Juu (Amekwezwa).”

  • *

    Maana yake “Baba wa Umati (Halaiki); Baba wa Wengi.”

Mwanzo 17:6

Marejeo

  • +Mwa 35:10, 11

Mwanzo 17:7

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yako.”

  • *

    Tnn., “mbegu yako.”

Marejeo

  • +Lu 1:72, 73

Mwanzo 17:8

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yako.”

Marejeo

  • +Kut 6:4; Ebr 11:8, 9
  • +Kum 14:2

Mwanzo 17:9

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yako.”

Mwanzo 17:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yako.”

Marejeo

  • +Mwa 21:4; Ro 2:29

Mwanzo 17:11

Marejeo

  • +Mdo 7:8; Ro 4:11

Mwanzo 17:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “mbegu yenu.”

Marejeo

  • +Lu 2:21

Mwanzo 17:13

Marejeo

  • +Kut 12:44

Mwanzo 17:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Huenda jina hili linamaanisha “Mgomvi.”

  • *

    Maana yake “Binti ya Mfalme.”

Marejeo

  • +Mwa 11:29

Mwanzo 17:16

Marejeo

  • +Mwa 18:10

Mwanzo 17:17

Marejeo

  • +Mwa 18:12
  • +Ro 4:19; Ebr 11:11

Mwanzo 17:18

Marejeo

  • +Mwa 16:11

Mwanzo 17:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Maana yake “Kicheko.”

  • *

    Tnn., “mbegu yake.”

Marejeo

  • +Mt 1:2
  • +Mwa 26:24

Mwanzo 17:20

Marejeo

  • +Mwa 16:10; 21:13, 18; 25:13-16; 1Nya 1:29-31

Mwanzo 17:21

Marejeo

  • +Mwa 26:3; Ebr 11:8, 9
  • +Mwa 18:10, 14; 21:1

Mwanzo 17:23

Marejeo

  • +Mwa 17:13

Mwanzo 17:24

Marejeo

  • +Mdo 7:8; Ro 4:11

Mwanzo 17:25

Marejeo

  • +Mwa 16:16

Jumla

Mwa. 17:2Mwa 15:18; Zb 105:8-11
Mwa. 17:2Mwa 22:17; Kum 1:10; Ebr 11:11, 12
Mwa. 17:4Zb 105:9-11
Mwa. 17:4Mwa 13:16; Ro 4:17
Mwa. 17:6Mwa 35:10, 11
Mwa. 17:7Lu 1:72, 73
Mwa. 17:8Kut 6:4; Ebr 11:8, 9
Mwa. 17:8Kum 14:2
Mwa. 17:10Mwa 21:4; Ro 2:29
Mwa. 17:11Mdo 7:8; Ro 4:11
Mwa. 17:12Lu 2:21
Mwa. 17:13Kut 12:44
Mwa. 17:15Mwa 11:29
Mwa. 17:16Mwa 18:10
Mwa. 17:17Mwa 18:12
Mwa. 17:17Ro 4:19; Ebr 11:11
Mwa. 17:18Mwa 16:11
Mwa. 17:19Mt 1:2
Mwa. 17:19Mwa 26:24
Mwa. 17:20Mwa 16:10; 21:13, 18; 25:13-16; 1Nya 1:29-31
Mwa. 17:21Mwa 26:3; Ebr 11:8, 9
Mwa. 17:21Mwa 18:10, 14; 21:1
Mwa. 17:23Mwa 17:13
Mwa. 17:24Mdo 7:8; Ro 4:11
Mwa. 17:25Mwa 16:16
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Mwanzo 17:1-27

Mwanzo

17 Abramu alipokuwa na umri wa miaka 99, Yehova alimtokea na kumwambia: “Mimi ni Mungu Mweza-Yote. Tembea mbele zangu na ujithibitishe mwenyewe kuwa bila kosa.* 2 Nitaimarisha agano langu kati yangu na wewe,+ nami nitawafanya wazao wako wawe wengi, wengi sana.”+

3 Ndipo Abramu akaanguka kifudifudi, na Mungu akaendelea kuongea naye, na kumwambia: 4 “Mimi nami, tazama! agano langu liko pamoja nawe,+ nawe hakika utakuwa baba wa mataifa mengi.+ 5 Jina lako halitakuwa tena Abramu;* jina lako litakuwa Abrahamu,* kwa sababu nitakufanya kuwa baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na wazao wengi, wengi sana, nami nitakufanya uwe mataifa, na wafalme watatoka kwako.+

7 “Nami nitalishika agano langu nililofanya pamoja nawe+ na uzao wako* baada yako katika vizazi vyao vyote; hili ni agano la milele, ili niwe Mungu wako na Mungu wa uzao wako* baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako* baada yako nchi ambamo uliishi ukiwa mgeni+—nchi yote ya Kanaani—iwe miliki ya kudumu, nami nitakuwa Mungu wao.”+

9 Mungu akaendelea kumwambia Abrahamu: “Wewe nawe, unapaswa kushika agano langu, wewe na uzao wako* baada yako katika vizazi vyao vyote. 10 Hili ndilo agano langu nililofanya pamoja nawe, ambalo wewe na uzao wako* baada yako mtalishika: Kila mwanamume miongoni mwenu ni lazima atahiriwe.+ 11 Ni lazima mtahiri nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati yangu nanyi.+ 12 Katika vizazi vyenu vyote, kila mwanamume miongoni mwenu mwenye umri wa siku nane ni lazima atahiriwe,+ yeyote anayezaliwa nyumbani mwenu na yeyote ambaye si mmoja wa uzao wenu* na yeyote aliyenunuliwa kwa pesa kutoka kwa mgeni. 13 Kila mwanamume aliyezaliwa nyumbani mwenu na kila mwanamume aliyenunuliwa kwa pesa zenu ni lazima atahiriwe,+ na agano langu katika miili yenu litakuwa agano la kudumu. 14 Ikiwa mwanamume yeyote ambaye hajatahiriwa hatatahiri nyama ya govi lake, ni lazima auawe. Amevunja agano langu.”

15 Kisha Mungu akamwambia Abrahamu: “Kuhusu mke wako Sarai,*+ usimwite tena Sarai, kwa sababu jina lake litakuwa Sara.* 16 Nitambariki na pia nitakupa mwana kupitia yeye;+ nitambariki Sara, naye atakuwa mataifa; wafalme wa mataifa watatoka kwake.” 17 Ndipo Abrahamu akaanguka kifudifudi, akaanza kucheka na kusema moyoni mwake:+ “Je, mwanamume mwenye umri wa miaka 100 atazaa mtoto, na je, Sara, mwanamke mwenye umri wa miaka 90, atazaa?”+

18 Kwa hiyo Abrahamu akamwambia Mungu wa kweli: “Afadhali umbariki Ishmaeli ili aendelee kuishi!”+ 19 Ndipo Mungu akasema: “Mke wako Sara hakika atakuzalia mwana, nawe unapaswa kumpa jina Isaka.*+ Nami nitaimarisha agano langu pamoja naye liwe agano la milele kwa uzao wake* baada yake.+ 20 Lakini kuhusu Ishmaeli, nimesikia ombi lako. Tazama! Nitambariki, nami nitamfanya awe na wazao wengi, nao wataongezeka na kuwa wengi, wengi sana. Atazaa wakuu 12, nami nitamfanya awe taifa kubwa.+ 21 Hata hivyo, nitaimarisha agano langu pamoja na Isaka,+ ambaye Sara atakuzalia wakati huuhuu mwaka ujao.”+

22 Mungu alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, alipanda na kumwacha Abrahamu. 23 Kisha Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwana wake na wanaume wote waliozaliwa nyumbani mwake na kila mwanamume aliyekuwa amemnunua kwa pesa, kila mwanamume katika nyumba ya Abrahamu, naye akawatahiri nyama ya magovi yao siku hiyohiyo, kama Mungu alivyokuwa amemwambia.+ 24 Abrahamu alikuwa na umri wa miaka 99 alipotahiriwa nyama ya govi lake.+ 25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka 13 alipotahiriwa nyama ya govi lake.+ 26 Siku hiyohiyo, Abrahamu alitahiriwa na pia Ishmaeli mwanawe. 27 Wanaume wote wa nyumba yake, yeyote aliyezaliwa nyumbani mwake na yeyote aliyenunuliwa kwa pesa kutoka kwa mgeni, walitahiriwa pia pamoja naye.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki