Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 20
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Mathayo—Yaliyomo

      • Wafanyakazi katika shamba la mizabibu wapokea mshahara unaolingana (1-16)

      • Kifo cha Yesu chatabiriwa tena (17-19)

      • Ombi la kupewa vyeo katika Ufalme (20-28)

        • Yesu atoa fidia kwa ajili ya wengi (28)

      • Wanaume wawili vipofu waponywa (29-34)

Mathayo 20:1

Marejeo

  • +Mt 21:33

Mathayo 20:2

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Nyongeza B14.

Mathayo 20:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, karibu saa 3 asubuhi.

Mathayo 20:5

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, karibu saa 6 mchana.

  • *

    Yaani, karibu saa 9 alasiri.

Mathayo 20:6

Maelezo ya Chini

  • *

    Yaani, karibu saa 11 jioni.

Mathayo 20:8

Marejeo

  • +Law 19:13; Kum 24:14, 15

Mathayo 20:9

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Nyongeza B14.

Mathayo 20:10

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Nyongeza B14.

Mathayo 20:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Angalia Nyongeza B14.

Marejeo

  • +Mt 20:2

Mathayo 20:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “ni baya; lina uovu.”

  • *

    Au “mkarimu.”

Marejeo

  • +Mt 6:23

Mathayo 20:16

Marejeo

  • +Mt 19:30; Mk 10:31; Lu 13:30

Mathayo 20:17

Marejeo

  • +Mk 10:32; Lu 18:31

Mathayo 20:18

Marejeo

  • +Mt 16:21; Mk 10:33, 34; Lu 9:22; 18:32, 33

Mathayo 20:19

Marejeo

  • +Mt 27:31; Yoh 19:1
  • +Mt 17:22, 23; 28:6; Mdo 10:40; 1Ko 15:4

Mathayo 20:20

Maelezo ya Chini

  • *

    Au, “akamwinamia.”

Marejeo

  • +Mt 4:21; 27:55, 56
  • +Mk 10:35-40

Mathayo 20:21

Marejeo

  • +Mt 19:28

Mathayo 20:22

Marejeo

  • +Mt 26:39; Mk 10:38; 14:36; Yoh 18:11

Mathayo 20:23

Marejeo

  • +Mdo 12:2; Ro 8:17; 2Ko 1:7; Ufu 1:9
  • +Mk 10:39, 40

Mathayo 20:24

Marejeo

  • +Mk 10:41-45; Lu 22:24

Mathayo 20:25

Marejeo

  • +Mk 10:42

Mathayo 20:26

Marejeo

  • +2Ko 1:24; 1Pe 5:3
  • +Mt 18:4; 23:11; Mk 10:43, 44; Lu 22:26

Mathayo 20:27

Marejeo

  • +Mk 9:35

Mathayo 20:28

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “nafsi yake.”

Marejeo

  • +Lu 22:27; Yoh 13:14; Flp 2:7
  • +Isa 53:11; Mk 10:45; 1Ti 2:5, 6; Tit 2:13, 14; Ebr 9:28

Mathayo 20:30

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “tuonyeshe rehema!”

Marejeo

  • +Mt 9:27; Mk 10:46-52; Lu 18:35-43

Mathayo 20:31

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “tuonyeshe rehema!”

Mathayo 20:34

Marejeo

  • +Mt 9:29

Jumla

Mt. 20:1Mt 21:33
Mt. 20:8Law 19:13; Kum 24:14, 15
Mt. 20:13Mt 20:2
Mt. 20:15Mt 6:23
Mt. 20:16Mt 19:30; Mk 10:31; Lu 13:30
Mt. 20:17Mk 10:32; Lu 18:31
Mt. 20:18Mt 16:21; Mk 10:33, 34; Lu 9:22; 18:32, 33
Mt. 20:19Mt 27:31; Yoh 19:1
Mt. 20:19Mt 17:22, 23; 28:6; Mdo 10:40; 1Ko 15:4
Mt. 20:20Mt 4:21; 27:55, 56
Mt. 20:20Mk 10:35-40
Mt. 20:21Mt 19:28
Mt. 20:22Mt 26:39; Mk 10:38; 14:36; Yoh 18:11
Mt. 20:23Mdo 12:2; Ro 8:17; 2Ko 1:7; Ufu 1:9
Mt. 20:23Mk 10:39, 40
Mt. 20:24Mk 10:41-45; Lu 22:24
Mt. 20:25Mk 10:42
Mt. 20:262Ko 1:24; 1Pe 5:3
Mt. 20:26Mt 18:4; 23:11; Mk 10:43, 44; Lu 22:26
Mt. 20:27Mk 9:35
Mt. 20:28Lu 22:27; Yoh 13:14; Flp 2:7
Mt. 20:28Isa 53:11; Mk 10:45; 1Ti 2:5, 6; Tit 2:13, 14; Ebr 9:28
Mt. 20:30Mt 9:27; Mk 10:46-52; Lu 18:35-43
Mt. 20:34Mt 9:29
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
  • 22
  • 23
  • 24
  • 25
  • 26
  • 27
  • 28
  • 29
  • 30
  • 31
  • 32
  • 33
  • 34
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Mathayo 20:1-34

Kulingana na Mathayo

20 “Kwa maana Ufalme wa mbinguni ni kama bwana mwenye nyumba aliyetoka asubuhi na mapema kwenda kuajiri wafanyakazi kwa ajili ya shamba lake la mizabibu.+ 2 Baada ya kukubaliana na wafanyakazi hao awalipe dinari* moja kwa siku, akawatuma katika shamba lake la mizabibu. 3 Akatoka pia karibu saa tatu,* akaona wengine wamesimama sokoni bila kazi; 4 akawaambia, ‘Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, nami nitawalipa haki yenu.’ 5 Basi wakaenda. Tena akatoka karibu saa sita* na saa tisa* na kufanya vivyo hivyo. 6 Mwishowe, akatoka karibu saa kumi na moja,* akakuta wengine wakiwa wamesimama tu, naye akawauliza, ‘Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?’ 7 Wakamjibu, ‘Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri.’ Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.’

8 “Ilipofika jioni, mwenye shamba la mizabibu akamwambia msimamizi wake, ‘Waite wafanyakazi uwalipe mshahara wao,+ ukianza na wa mwisho na kumalizia na wa kwanza.’ 9 Wale watu wa saa 11 walipokuja, wakapokea kila mmoja dinari* moja.⁠ 10 Basi, wale wa kwanza walipokuja, walidhani wangepokea zaidi; lakini wao pia wakalipwa dinari* moja. 11 Walipoipokea wakaanza kumlalamikia bwana mwenye nyumba 12 na kusema, ‘Watu hawa wa mwisho walifanya kazi kwa saa moja tu; na bado umewalipa sawa na sisi tuliofanya kazi ngumu mchana kutwa kwenye jua kali!’ 13 Lakini akamjibu mmoja wao, akasema, ‘Mwenzangu, sijakukosea. Tulikubaliana dinari* moja, sivyo?+ 14 Chukua mshahara wako uende. Ninataka kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. 15 Je, sina haki ya kufanya kile ninachotaka na vitu vyangu? Au jicho lako lina wivu* kwa sababu mimi ni mwema?’*+ 16 Vivyo hivyo, wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”+

17 Alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, Yesu akawaita faraghani wale wanafunzi 12 na kuwaambia wakiwa barabarani:+ 18 “Tazama! Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa binadamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi. Nao watamhukumia kifo+ 19 na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa ili wamdhihaki, wampige mijeledi, na kumuua kwenye mti;+ na siku ya tatu atafufuliwa.”+

20 Ndipo mama ya wana wa Zebedayo+ akamjia akiwa na wanawe, akamsujudia* na kumwomba jambo fulani.+ 21 Yesu akamuuliza: “Unataka nini?” Akamjibu: “Toa agizo kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto, katika Ufalme wako.”+ 22 Yesu akajibu: “Hamjui kile mnachoomba. Je, mnaweza kunywa kikombe ambacho niko karibu kukinywa?”+ Wakamwambia: “Tunaweza.” 23 Akawaambia: “Kwa kweli mtakunywa kikombe changu,+ lakini kuketi upande wangu wa kuume na upande wangu wa kushoto si haki yangu kutoa, bali wataketi wale ambao Baba yangu amewatayarishia.”+

24 Wale wengine kumi waliposikia jambo hilo, wakawakasirikia hao ndugu wawili.+ 25 Lakini Yesu akawaita, akawaambia: “Mnajua kwamba watawala wa mataifa hupiga ubwana juu yao na wakuu hutumia mamlaka juu yao.+ 26 Haipaswi kuwa hivyo kati yenu;+ bali yeyote anayetaka kuwa mkubwa kati yenu lazima awe mhudumu wenu,+ 27 na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu lazima awe mtumwa wenu.+⁠ 28 Kama vile Mwana wa binadamu alivyokuja, si kuhudumiwa, bali kuhudumu+ na kutoa uhai wake* uwe fidia badala ya wengi.”+

29 Walipokuwa wakitoka Yeriko umati mkubwa ukamfuata. 30 Na tazama! wanaume wawili vipofu waliokuwa wameketi kando ya barabara waliposikia kwamba Yesu anapitia hapo, wakapaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”*+ 31 Hata hivyo, umati ukawakemea na kuwaambia wanyamaze; lakini wakapaza sauti hata zaidi, wakisema: “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”* 32 Basi Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza: “Mnataka niwafanyie nini?” 33 Wakamjibu: “Bwana, tunaomba macho yetu yafunguliwe.” 34 Yesu akawasikitikia, akayagusa macho yao,+ na mara moja wakaanza kuona, nao wakamfuata.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki